Nafasi ya Mwingiliano Fani katika Kukuza Fasihi ya Watoto
Keywords:
Mwingiliano, Fani, Fasihi ya Watoto, UmuundoAbstract
Makala haya yanahusu jinsi vipengele vya fani vinavyotumiwa katika vitabu vya fasihi ya watoto ili kufanikisha malengo ya waandishi. Utafiti uliofanywa uliongozwa na nadharia ya Umuundo iliyoasisiwa na Ferdinand De Saussure (1916). Nadharia hii inajibainisha kwa kuangalia ujumla wa uhusiano wa sehemu moja kwa nyingine katika kufanya kitu kizima. Kwa kuongozwa na nadharia hii tulichukulia fasihi kuwa kitu kizima kinachojengwa kwa maudhui na fani. Katika ngazi ya pili fani nayo imeundwa kwa vipengele mbalimbali vya lugha kama vile methali, misemo, nahau, taswira, picha na tashbihi. Vipengele hivi vilitambuliwa na matumizi yavyo yakafafanuliwa na kuelezwa. Utafiti huu uliteua kimakusudi riwaya za Kisasi Hapana, Nimefufuka, Sitaki Iwe Siri, na Wema wa Mwanakatika kuchunguza jinsi mwingiliano fani unavyofanikisha kazi za fasihi zinazolenga watoto.