Dhima ya Fasihi katika Mshikamano wa Kitaifa

Tathmini ya Tungo za Tom Olali

Authors

  • Mwenda Mbatiah Chuo Kikuu Nairobi Author

Keywords:

Dhima, Fasihi, Mshikamano, Kitaifa

Abstract

Makala haya yanajadili suala la dhima ya fasihi katika kuleta mshikamano wa kitaifa. Hili ni suala zito barani Afrika, ambapo mchakato wa kujenga utaifa ulioanza katika harakati za ukombozi, unakabiliwa na changamoto nyingi. Nchini Kenya, kwa mfano, tumeshuhudia matukio kadha ambayo yametishia kuliporomosha taifa lililozaliwa mwaka wa 1963. Mfano mzuri ni vurugu ya baada ya uchaguzi mwaka wa 2007 hadi 2008. Msimamo wetu ni kwamba fasihi ya kitaifa inaweza kutoa mchango muhimu katika kuleta mshikamano wa kitaifa na amani ya kudumu. Lakini swali ni je, ni fasihi ya aina gani inayoweza kufanikisha hilo? Katika kutafuta jawabu la swali hilo, tunazitathmini kazi za Tom Olali, ambaye ni mmojawapo wa waandishi wa Kiswahili nchini Kenya. Kazi zinazohusika ni: Mafamba (2008), Watu wa Gehenna (2012) na Mashetani wa Alepo (2015). Tumetathmini vipengele vya fani na maudhui ya kazi hizo mintarafu ya mada ya iliyotajwa hapo juu.

Downloads

Published

30-06-2019

Issue

Section

Articles