Uchunguzi wa Sababu za Mtumizi ya Lakabu za Wanafunzi katika Ufundishaji na Ujifunzaji wa Kiswahili kama Lugha ya Kigeni Nchini Tanzania

Authors

  • Joyce Henock Nyiti Idara ya Elimu Sekondari Meru Author
  • Adventina Buberwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Author

Keywords:

Sababu, Lakabu za Wanafunzi, Lugha ya Kigeni, Ufundishaji, Ujifunzaji

Abstract

Miongoni mwa maeneo ambayo lakabu hutumika ni katika ufundishaji na ujifunzaji wa lugha ya kigeni. Tafiti mbalimbali zimefanyika kuhusu matumizi ya lakabu katika ufundishaji na ujifunzaji wa Lgn na kubainisha sababu mbalimbali za kutumia lakabu katika ufundishaji wa lugha kwa ujumla. Licha ya kubainisha sababu hizo, tafiti hizo ziliangazia lugha mbalimbali bila kuangazia sababu za matumizi ya lakabu za wanafunzi katika ufundishaji na ujifunzaji wa Lgn mahususi. Makala haya yameshughulikia sababu za matumizi ya lakabu za wanafunzi katika ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili kama Lgn nchini Tanzania. Data za utafiti huu zimekusanywa kutoka kwa walimu 6 wanaofundisha Kiswahili kama Lgn na wanafunzi 15 kutoka katika vyuo/taasisi 03 nchini Tanzania ambazo ni Taasisi ya Kiswahili na Utamaduni (KIU), Chuo cha Maendeleo na Ushirikiano wa Kimataifa (MS TCDC) na Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA). Data zimekusanywa kwa mbinu ya usaili na kuwasilishwa kimaudhui kisha zikatolewa maelezo yaliyoongozwa na Modeli ya Elimu ya Kijamii ya Robert C. Gardner, 2005. Sababu zilizobainika katika matokeo hayo ni pamoja na kuwapa wanafunzi utambulisho, kupata urahisi wa kuwakumbuka wanafunzi kwa lakabu zao, kuchochea motisha ya wanafunzi katika ujifunzaji wa Kiswahili kama Lgn, kurahisisha ufundishaji wa sarufi, kukidhi kipengele cha kiutamaduni, kuepuka makosa ya matamshi ya majina ya wanafunzi na kutumia lakabu kwa sababu tu ni utaratibu wa chuo/taasisi husika. Makala haya yanapendekeza kuwapa walimu mafunzo kuhusu matumizi ya lakabu ili watambue faida zake katika ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili kama Lgn. Pia, wito unatolewa na makala haya kwa wataalamu wengine kuchunguza madhara ya kutumia lakabu zisizofaa katika ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni ili waweke bayana maarifa hayo.

References

Agyekum, K. (2006). The Sociolinguistic of Akan Personal Names. Nordic Journal of African Studies, 15(2), 206-235.

Atolagbe, D., Abegunde, C., & Morofonfoye, O. (2015). Generation and Attribution of Nicknames among Secondary School Students: Indices of Linguistic Creativity. Research on Humanities and Social Sciences, 5(20), 104-109.

Bobrova, M. (2022). Nicknames in Teaching Russian as a Foreign Language. Russian Language Studies, 20(1), 22-34. Inapatikana katika DOI 10.22363/2618-8163-2022-20-1-22-34.

Diao, W. (2014). Between Ethnic and English Names: Name Choice for Transnational Chinese Students in a US Academic Community. Journal of International Students, 4(3), 205-222. Inapatikana katika http://jistudents.org.

Filani na Melefa (2014). A Socio-Semiotic Study of Nicknaming among Undergraduates katika Chuo Kikuu cha Naijeria. Linguistik Online, 68(6), 22-42. Inapatikana katika http://dx.doi.org/10.13092/lo.68.1632.

Garayeva, A. K., Akhmetzyanov, I. G., & Khismatullina, L. G. (2016). The Significance of Learning Nicknames fo Public Figures in Modern English and American Language Models of the World. International Journal of Environmental and Science Education, 11(4), 10337-10345.

Gardener, R. C., & Macltyre, P. C. (1993). A Student’s Contributions to Second Language Learning. Part II: Affective Variables. Language Teaching, 26, 1-11. Inapatikana katika http://dx.doi.org/10.1017/S0261444800000045.

Gardner, C. R. (2000). Correlation, Causation, Motivation and Second Language Acquisition. Canadian Psychology, 41, 1-24. http://dx.doi.org/10.1037/h0086854.

Gardner, R. C. (1985). Social Psychology and Second Language Learning: The Role of Attitudes na Motivation. London: Edward Arnold Publishers.

Glenz, T. (2014). The Importance of Knowing Students’ Names. Journal on Best Teaching Practice, 21-22.

Jamalvandi, B., & Jamalvandi, A. (2016). Application of Nicknames among Ilami Kurdish Students, West of Iran. ResearchGate/Sociology Study?, 6(9), 604-614. Inapatikana katika doi:10.17265/2159-5526/2016.09.006.

Kennedy na Zamuner. (2006). Nicknames and the Lexicon of Sports. American Speech, 81(4), 387- 422.

Koehn, S. C. (2015). Use of Self-selected Nicknames by Female Kuwaiti Students and their Perception of the Impact of Nicknames up on their Learning in the Classroom. Near and Middle Eastern Journal of Research in Education. Inapatikana katika http://dx.doi.org/10.5339/nmejre.2015.2.

Kuranchie, A. (2012). Student’s Nicknames: Their Source and Effects on Learning. Journal of Education and Practice, 3(14), 23- 41.

Lakaw, A. (2006). Hiding Behind Nicknames: A Linguistc Study of Anonymity in IRC Chatrooms. Student Thesis. Vaxjo University. Inapatikana katika http://Inu.diva-portal.org/smash/record.jsf?pid=diva2:206935.

Mapunda, G. (2014). What Do My Students Call Me? Nicknaming of Lecturers by Students at the University of Dar es Salaam. Journal of Linguistics and Language in Education, 8(1), 90-107.

Mensah, E. O., & Ndimele, R. I. (2020). King Shumba, Smilling Devil and Baby Doctor: A Sociolinguistic Study of Lecturers’ Nicknames in Two Nigerian Universities. African Identities. Inapatikana katika DOL: 10. 1080/14725843.2020.1813544.

Mphande, L. (2006). Naming and Linguistic Africanism in African American Culture. In Mugane, J. P. (Ed.), Selected Proceedings of the 35th Annual Conference on African Linguisticsed (104-113). Somerville, MA: Cascadilla Proceedings Project.

Oxford, R. (2003). Language Learning Style and Strategies. USA: Cambridge University Press.

Reyes, M., & Rodriguez, J. (2006). Teaching English in Mixed-ability Classrooms: Some Teachers’ Thoughts on Responding to the Needs of all Learners. Inapatikana katika www.teaching.english.org.uk.

Saleh, F. H. (2019). Changamoto za Ufundishaji na Ujifunzaji wa Kiswahili kama Lugha ya Kigeni katika Darasa Mseto la Wingilugha. Tasnifu ya Shahada ya Uzamili ya Elimu katika Ufundishaji wa Kiswahili kwa Wazungumzaji wa Lugha Nyingine (M.Ed.TEKSOL) Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar.

Sobane, K. (2016). The Pragmatics of Nicknames Students Use for their Lecturers. Inapatikana katika https://www.researchgate.net/publication/292149459.

Starks, D., & Taylor-Leech, K. (2021). A Research Project on Nicknames and Adolescent Identities. New Zealand Studies in Applied Linguistics, 17(2), 87-97.

Wa’Njogu. (2008). Ufundishaji wa Kiswahili Marekani: Maendeleo na Changamoto. Swahili Forum, 15, 121-133.

Xinran, W. (2023). Stories of Names: Exploring Chines High School Language-other-than-English Learners’ Foreign Name(s) Usage and its Role in Multilingual Identity Construction. Journal of Multilingual and Multicultural Development, 1-15. Inapatikana katika DOI: 10,1080/01434632.2023,2170392.

Yi, Q. (2010). Culture Understanding in Foreign Language Teaching. Canadian Centre of Science and Education, 3(4), 58-61.

Yule, G. (2010). The Study of Language. United Kingdom: Cambridge University Press.

Downloads

Published

30-04-2025

Issue

Section

Articles

How to Cite

Uchunguzi wa Sababu za Mtumizi ya Lakabu za Wanafunzi katika Ufundishaji na Ujifunzaji wa Kiswahili kama Lugha ya Kigeni Nchini Tanzania. (2025). Mwanga Wa Lugha, 10(1), 101-109. https://journals.mu.ac.ke/index.php/mwl/article/view/549