Tafsiri Tenge za Dhana Asilia za Kiswahili kwenye Lugha ya Kiingereza katika Vyombo vya Habari
Keywords:
Tafsiri Tenge, Dhana Asilia, Kiingereza, Vyombo vya HabariAbstract
Vyombo vya habari ni asasi muhimu katika kufikisha ujumbe kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine. Vyombo hivyo ni televesheni, magazeti, idhaa za redio, mitandao ya kijamii n.k (Kambaya, 2022). Nyenzo kubwa itumiwayo na vyombo vya habari katika kuhakikisha ujumbe unafika kwa wakati na kwa ufasaha uliokusudiwa ni lugha. Hapa tunazungumzia lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, makala haya yanalenga kuonesha mtindo unaozidi kushamiri wa kufasiri dhana asilia za Kiswahili kwa kuegemea lugha ya Kiingereza, taathira zake na kutoa mazingatio muhimu kwa vyombo vya habari. Nadharia ya tafsiri iliongoza uchunguzi huu. Data zilikusanywa kwa njia ya maktabani kwa kupitia kwa umakini maandiko mbalimbali, ushuhuduaji na usaili. Matokeo yamedhihirisha kuwa kuna tafsiri za kiholela ambazo hufanywa haraka haraka zinazoweza kuingiza ruwaza tenge zenye ukakasi katika lugha ya Kiswahili. Mathalan, kusema mwisho wa siku kwa tafsiri ya at the end of the day badala ya hatimaye, Imebainika pia, kukithiri kwa utenge huu kunaweza kuleta athari ya kuwa na ‘Kiswanglish’-yaani Kiswahili kilichochanganyika na Kiingereza au Kiswahili cha Kiingereza. Vilevile, makala inapendekeza mazingatio muhimu ya kuboresha mazao ya tafsiri katika vyombo vya habari kuwa ni; wafasiri katika vyombo vya habari wawe weledi,watumie istilahi sanifu za Kiswahili kwa kujiamini, waendeleze dhima ya kutangaza marekebisho ya tafsiri tenge za Kiswahili, washirikiane na wataalamu wafasiri kutoka vyombo vya ukuzaji wa Kiswahili na wasilazimishe kutafsiri dhana za utamaduni na mila za kigeni katika Kiswahili. Makala yanatoa mchango katika uga wa tafsiri na maendeleo ya Kiswahili.
References
BAKITA, (2029). Kamusi Kuu ya Kiswahili, Nairobi, Longhorn Publishers Ltd.
BAKIZA, (2010). Kamusi la Kiswahili Fasaha. Nairobi: Oxford University Press.
Eliah.V. (2019). Kiswahili katika Vyombo vya Habari: Ndani na Nje ya Tanzania, Dar es Salaam, TATAKI.
Dadi, K. S. (1995). “Dhima ya Vyombo vya Habari katika Matumizi ya Msamiati”, katika Mlacha (Mh.) Kiswahili na Vyombo vya Habari. Dar es Salaam: TUKI.
Emmanuel, E. O. (2011). “The Impact of Pragmatic Competence in Traslation: The case of BBC English Kiswahili World News Traslations”, Tasinifu ya Umahiri,(Haijachapishwa) Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Fupi, R. (2010). “A Critique of Electronic Media Tranlations: A Case Study of TBC (Television) English Swahili News Translations”, Tasinifu ya Umahiri, (Haijachapishwa) Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Jilala, H. (2014) “Athari za Kitamaduni katika Tafsiri: Mifano kutoka Matini za Kitalii katika Makumbusho za Tanzania”. Tasinifu ya Uzamivu (Haijachapishwa). Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dar es Salaam.
Harris, R.J. (1989). A Cognitive Psychology of Mass Communication, Lawrence New Jersey. London. Earlbaum Associates Publishers.
Kambaya, M. (2022). “Nafasi ya Redio katika Kujenga Umoja wa Afrika kupitia Lugha ya Kiswahili: Uzoefu wa Redio One” katika Kiswahili katika Anga za Kimataifa, Julai 7, Siku ya Kiswahili Duniani. (Mtesigwa P. na Duwe. E) (Wah.) Dar es Salaam: TUKI na BAKITA.
Kiganya, W. (1995). “Sera ya Kiswahili, Mafanikio na Matatizo Nchini Kenya”, katika Mlacha Mh.) Kiswahili katika Kanda ya Afrika Mashariki. Dar es Salaam:TUKI.
Kiango, J.G. (2008). Ukuzaji wa Istilahi za Kiswahili. Dar es Salaam: TUKI.
Khan, N. I. (2019). Case Study as a Method of Qualitative Research. Qualitative Techniques for workplace Data Analysis (kur.170-196). IGI Global. Inapatikana katika http://www.igi-global.com/chapter/case-study-as-a-method-of-qualitative-research/207797. Ilisomwa tarehe 15/2/2019.
Makunja, G. S. (1995). “Sarufi na Msamiati wa Kiswahili katika Vyombo vya Habari”, katika Mlacha (mh.) Kiswahili na Vyombo vya Habari. Dar es Salaam:TUKI.
Mohochi, E. S. (2006). “Kiswahili na Vyombo vya Habari nchini Kenya: Makosa katika Matumizi ya Lugha” katika Kiswahili. Juz 69. (Massamba, D.P.B) (Mh) Dar es Salaam: TUKI.
Mrikaria, G. na Ngesu, S.N. (2022). “Tafsiri kama Nyenzo ya Kutandawaza Utamaduni wa Mswahili: Mfano wa Siku njema (1996) na A Good Day (2019) katika Kiswahili. Juz 85 (2) (Mnenuka na Mpemba) (Wah.) Dar es Salaam. TUKI.
Mwansoko, H. J. M. (2021) Misingi ya Kukuza Kiswahili Kimataifa, Mhadhara wa Uzinduzi wa Uprofesa, Mbeya, Chuo Kikuu Teofilo Kisanji.
Mwansoko, H. J. M., Mekacha, R.D.K., Masoko, D.L.W. na Mtesigwa, P.C.K (2015). Kitangulizi cha Tafsiri: Nadharia na Mbinu. Dar es Salaam: TUKI.
Mwansoko, H. J. M. (1995). “Dhima ya Vyombo vya Habari katika Ukuzaji, Usanifishaji na Uenezaji wa Istilahi”, katika, Mlacha (mh.) Kiswahili na Vyombo vya Habari. Dar es Salaam: TUKI.
Riazi, A.M. (2018). “Mixed Methods Approaches to Studying Second Language Writing”. The TESOS Encyclopaedia of English Language Teaching, kur.1-6.
TATAKI, (2014) Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Dar es Salaam: Oxford University Press.
TUKI, (2013). Kamusi ya Kiswahili Sanifu, (Toleo la 3). Nairobi: Oxford University Press: Nairobi.
Waliibora, K.W (2001) “Matatizo ya Taarifa katika Vyombo vya Habari” katika Kiswahili, Dar es Salaam, TUKI, Juz.64:23-30.
Vituo vya Televisheni na Magazeti Mbalimbali.