Vijenzi vya Uduara katika Sanaa za Maonyesho za Jamii ya Wangoni

Authors

  • Athumani S. Ponera Chuo Kikuu cha Dodoma Author
  • Martina Duwe Chuo Kikuu cha Dodoma Author

Keywords:

Uduara, Vijenzi vya Uduara, Falsafa ya Kiafrika

Abstract

Makala haya yanafafanua vijenzi vinavyouunda na kuushikilia uduara kama kipengele kimojawapo maarufu cha falsafa ya Kiafrika. Hoja kuu ya makala ni kudhihirisha kuwapo kwa dhana ya uduara katika sanaa za maonyesho za jamii ya Wangoni. Makala haya ni sehemu tu ya matokeo ya uchunguzi mpana uliofanyika katika jamii ya Wangoni kuhusu dhana ya uduara. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu tatu ambazo ni usaili, ushuhudiaji wa utendekaji wa shughuli mbalimbali za kijamii, pamoja na udurusu wa kimaktaba. Makala yana sehemu tano. Sehemu ya kwanza ni utangulizi; ambapo dhana za msingi zinazoyajenga makala zimedokezwa. Sehemu ya pili inafafanua vijenzi vya dhana ya uduara. Sehemu ya tatu inahusu tija za dhana ya uduara. Sehemu ya nne ni hitimisho, na sehemu ya tano ni marejeleo. Kwa ujumla, mjadala wetu umeonyesha kuwa sehemu kubwa ya matukio, matendo na vitu vinavyohusiana na Wangoni hufanywa au kuundwa kwa umbo la duara. Katika makala haya, matukio, matendo na vitu hivyo, vimeelezwa kama ni vijenzi. Vijenzi hivyo ni vitatu. Navyo ni: uchezaji wa ngoma, michezo ya watoto, pamoja na ujumi wao unaojidhihirisha kupitia vifaa mbalimbali vya kutekelezea sanaa za maonyesho.

Downloads

Published

30-04-2018

Issue

Section

Articles