Matatizo ya Uchanganuzi wa Sentensi za Kiswahili kwa Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Tanzania
Keywords:
Uchanganuzi, Sentensi za Kiswahili, Sekondari, Upili wa Chini, Upili wa JuuAbstract
Ufundishaji wa sintaksia katika vyuo vikuu nchini Tanzania unakabiliwa na matatizo ya kinadharia na kimaudhui (Kahigi na Hassan, 2020). Wahitimu wa vyuo vikuu hufanya kazi ya kufundisha wanafunzi wa somo la Kiswahili katika shule za sekondari nchini Tanzania. Miongoni mwa mada zinazofundishwa katika somo la Kiswahili ni uchanganuzi wa sentensi. Matatizo ya kinadharia na kimaudhui wanayohitimu nayo walimu hao huvukizwa katika ufundishaji wa uchanganuzi wa sentensi. Kwa hiyo, makala haya yalichunguza matatizo ya uchanganuzi wa sentensi za Kiswahili kwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini Tanzania. Utafiti huu umefanyikia uwandani na maktabani. Mbinu iliyotumika kukusanya data za maktabani ni usomaji matini ilhali hojaji na jaribio zilitumika kukusanya data za uwandani. Data zilikusanywa kutoka shule 20 za sekondari nchini Tanzania (16 za bara na 4 za Zanzibar). Katika shule hizo, 10 zilikuwa za upili wa chini na 10 za upili juu. Mkabala wa kitaamuli ulitumika katika kuchambua data za utafiti huu. Data zilizokusanywa zilichanganuliwa kwa kuongozwa na Mkabala wa Kileksika ulioasisiwa na Lewis (1993). Matatizo yaliyobainika ni ugawanyaji wa mti-matawi katika matawi zaidi ya mawili, ukosefu wa maarifa kuhusu nadharia za uchanganuzi wa sentensi, dosari za uainishaji wa maneno, ubainishaji wa neno zaidi ya moja kama aina moja ya neno na uchanganyaji wa vipashio vya uchanganuzi. Baadhi ya vyanzo vya matatizo hayo ni dosari katika miongozo ya ufundishaji, vitabu na uhaba wa maarifa kwa waalimu wa sarufi katika shule za sekondari. Utafiti unapendekeza maboresho ya vitabu vya kiada na ziada, miongozo na mafunzo elekezi kwa waalimu wa sarufi katika shule za sekondari.
References
Hassan, F. (2021). Mikabala ya Uchanganuzi wa Viambajengo vya Sentensi na Istilahi Zinazotumika: Mifano kutoka Lugha ya Kiswahili. Mulika, 40(2), 1-22.
John, J. (2011). Kiswahili Kidato cha Tatu: Kitabu cha Mwanafunzi (Toleo la 2). Dar es Salaam: Oxford University Press Tanzania Ltd.
John, J. na Mduda, F. (2012). Kiswahili Kitado cha Tano na Sita: Kitabu cha Mwanafunzi. Dar es Salaam: Oxford University Press (T) Ltd.
Kahigi, K. K. na Hassan, F. (2020). Matatizo ya Ufundishaji wa Sintaksia katika Vyuo Vikuu Nchini Tanzania. Jarida la Mnyampala, 1, 105-120.
Kayne, R. S. (1994). Antisymmetry in Syntax. Cambridge MA: The MIT Press.
Lewis, M. (1993). The Lexical Approach: State of ELT and a Way Forward. Hove: Language Teaching Publications.
Masebo, J. A. Na Nyangwine, N. C. M. (2016). Nadharia ya Lugha-Kiswahili 1: Kidato cha 5 na 6. Dar es Salaam: Nyambari Nyangwine Publishers.
Massamba, D. P. B., Kihore, Y. M. na Hokororo, J. I. (2012). Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu (SAMIKISA): Sekondari na Vyuo (Chapa ya Nne). Dar es Salaam: TUKI.
Matinde, R. S. (2012). Dafina ya Lugha, Isimu na Nadharia Kwa Sekondari, Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu. Mwanza: Serengeti Educational Publisher Limited.
Mohamed, A. M. (1986). Sarufi Mpya. Dar es Salaam: Dar es Salaam Press and Publicity Centre.
Ndumiwe, E. J. (2020). Kurunzi ya Isimu na Muundo wa Kiswahili. Mwanza: Tridax Africa Company Limited.
Ndumiwe, E. J. (2022). Utelezi wa Uainishaji wa Baadhi ya Maneno ya Kiswahili: Kigezo cha Kimofosintaksia. Jarida la Fahari ya Kiswahili, 1(1), 92 - 104.
Nkwera, F. M. (1978). Sarufi na Fasihi: Sekondari na Vyuo. Dar es Salaam: Tanzania Publishing House.
Saluhaya, M. C. (2016). Kiswahili-1: Nadharia ya Lugha, Kidato cha Tano, Sita na Elimu ya Juu. Dar es Salaam: Ahmadiyya Printing Press.
TET. (1988). Kiswahili Sekondari. Dar es Salaam: Short Prints.
TET. (2021). Kiswahili Shule za Sekondari: Kitabu cha Mwanafunzi Kidato cha Tatu. Dar es Salaam: Taasisi ya Elimu Tanzania.
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. (2005). Muhtasari wa Somo la Kiswahili kwa Elimu ya Sekondari: Kidato cha I-IV. Dar es Salaam: TET.
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. (2010). Muhtasari wa Kiswahili kwa Elimu ya Sekondari: Kidato cha V-VI. Dar es Salaam: TET.