Mchango wa Mbinu ya Familia Wenyeji katika Ufundishaji na Ujifunzaji wa Kiswahili kama Lugha ya Kigeni
Keywords:
Kiswahili, Lugha ya Kigeni, Kijalizo, KiambajengoAbstract
Kijalizo na kiegesho ni viambajengo ambavyo vimeelezwa na wataalamu mbalimbali. Kijalizo kinaweza kurejelewa kama kiambajengo muhimu cha sentensi au kishazi ambacho huwa na kazi ya kukamilisha maelezo ya msingi katika neno, kirai au sentensi. Kiegesho ni kiambajengo kisichokuwa na uhusiano wa moja kwa moja na maneno mengine kisintaksia bali hufanya kazi ya kutoa taarifa za ziada katika neno au kundi la maneno. Kwa hiyo vijalizo na viegesho ni vipashio muhimu katika kutoa taarifa za msingi na za ziada kuhusu sentensi. Maandiko ya wataalamu mbalimbali yamepelekea kuchanganywa kwa dhana hizi mbili, hasa katika kuvielezea vipashio hivyo katika utokeaji wake kinafasi katika sentensi za Kiswahili. Hii ni kwa sababu kuna wakati kijalizo huonekana kama kiegesho na wakati mwingine kiegesho ni kama kijalizo. Makala haya yakiongozwa na nadharia ya Eksibaa yamekusudia kubainisha zaidi kati ya kijalizo na kiegesho kwa kuchunguza makutano na mwachano wa vijalizo na viegesho katika sentensi za Kiswahili. Yaani wakati gani vipashio hivyo hujitokeza pamoja katika sentensi na wakati gani haviwezi kutokea pamoja katika sentensi. Imegundulika kuwa vipashio hivyo hukutana katika mfuatano wa miundo maalumu ya virai na huachana kulingana na mifuatano hiyo maalumu katika sentensi za Kiswahili kwa mkabala wa kimuundo.