Nafasi ya Wahusika Jumui katika Ujenzi wa Maudhui

Mifano kutoka Riwaya za Kimajaribio za Kiswahili

Authors

  • Joyce A. Obetch Chuo Kikuu cha Rongo Author
  • James O. Ontieri Chuo Kikuu cha Rongo Author
  • Mark A. Odawo Chuo Kikuu cha Rongo Author

Keywords:

Maudhui, Riwaya za Kimajaribio, Wahusika Jumui

Abstract

Utunzi wa kazi za sanaa huhitaji ustadi mkubwa katika uteuzi na usawiri wa wahusika. Kutokana na umuhimu wao katika kazi yoyote ile ya fasihi, wahusika husawiriwa kisanaa na mwandishi ili waweze kufanikisha ujenzi wa maudhui na vilevile kuwakilisha dhana mbalimbali zinazoakisi maisha katika jamii (Msokile, 1992). Tafiti nyingi zimefanywa kuhusu usawiri wa wahusika jumui katika riwaya za Kiswahili za kimajaribio lakini kwa uelewa wetu, nafasi ya wahusika jumui katika ujenzi wa maudhui haijashughulikiwa kikamilifu. Kwa mujibu wa hoja hii, makala haya yanajadili jinsi usawiri wa wahusika jumui katika riwaya teule za kimajaribio za Babu Alipofufuka (2001) na Dunia Yao (2006) unavyowasilisha maudhui ya kihalisia. Riwaya hizi ziliteuliwa kimaksudi kutokana na uwezo wake wa kutoa data yakini zilizotosheleza mahitaji ya utafiti huu. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya usomaji makini wa riwaya teule, kisha zikachanganuliwa na kuwasilishwa kwa njia ya maelezo ya kinathari. Utafiti ulionesha kuwa wahusika jumui wametumiwa kujenga maudhui ya utandawazi, utamaduni mpya, utabaka, uongozi mbaya na sanaa mpya katika riwaya teule. Matokeo haya yataongeza maarifa ya uhakiki wa kitaaluma wa kazi za fasihi na utunzi wa kiubunifu.

References

Alomo, O. S. (2016). Uwakilishaji wa Utandawazi katika Riwaya Mpya ya Kiswahili Iliyoandikwa na S. A. Mohammed na K. W. Wamitila (Tasnifu ya Uzamili). Chuo Kikuu cha Egerton.

Althusser, L. (1968). Reading Capital. Paris: Librairie Francois Maspero.

Barry, P. (2002). Beginning Theory. Manchester: Manchester University Press.

Baudrillard, J. (1983). Simulations. New York: Semiotext(e).

Bergonzi, B. (1972). The Situation of the Novel. London: Penguin Publishers.

Brake, M. (1980). The Society of Youth Culture and Youth Subcultures: Sex, Drugs and Rock ‘n’ Roll? London: Routledge and Kegan Paul.

Friedman, T. L. (2005). The World is Flat: A Brief History of the Twenty-First Century. New York: Farrar Straus and Giroux.

Gromov, M. D. (1998). Nagona and Mzingile Novels, Tale or Parable? Swahili Forum, 5(55), 73-78.

Jerono, P. (2016). Taaluma ya Uanahabari na Kiswahili katika Enzi ya Utandawazi. L. C. Mwita. (Mh.). Kiswahili na Utandawazi. Nairobi: Twaeza Communications, 105-115.

Kamunde, M. (1983). Kilio cha Wanyonge katika Riwaya za Said Ahmed Mohamed. (Tasnifu ya Uzamili) (Haijachapishwa). Chuo Kikuu cha Nairobi.

Kamusi ya Karne ya 21 (2011). (Toleo la Pili). Nairobi: Longhorn Publishers.

Kenan, R. S. (1983). Narrative Fiction: Contemporary Poetics. London: Routledge.

Khamis, S. A. M. (2017). Vionjo vya Riwaya Mpya ya Kiswahili. Kioo cha Lugha, 5(1), 13-23.

Lee, G. (2004). A Million Little Choices: The ABCs of CNF. London: Yale University Press.

Marx, K. (1973). On Literature and Art. New York: International General.

Mbiti, J. S. (2010). Introduction to African Religion. Kampala: East African Educational Publishers, Ltd.

Mbiti, J. S. (2011). African Religion and Philosophy. Kampala: East African Educational Publishers Ltd.

Mohamed, S. A. (2001). Babu Alipofufuka. Nairobi: Oxford University Press, East Africa Ltd.

Mohamed, S. A. (2006). Dunia Yao. Nairobi: Oxford University Press, East Africa Ltd.

Mulokozi, M. M. (1996). Fasihi ya Kiswahili. Dar es Salaam: Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Mwamzandi, I. Y. (2013). Riwaya Teule za Karne ya Ishirini na Moja na Udurusu wa Nadharia ya Fasihi. Swahili Forum, 20, 48-66.

Roh, F. (1925). Magic Realism: Post–Expressionism. Magical Realism, Theory, History, Community. Durham: Duke University Press.

Selfe, P. (1993). Alevel Sociology: Trends and Patterns (2nd Ed.). London: Macmillan Press Ltd.

Senkoro, F. E. M. K. (2007). Uhalisiamazingaombwe katika Fasihi ya Kiswahili: Istilahi Mpya, Mtindo Mkongwe. Kioo cha Lugha, 5, 1-12.

Tempels, P. (1959). Bantu Philosophy. Paris: Presence Africaine.

TUKI (2013). Kamusi ya Kiswahili Sanifu (Toleo la Tatu). Dar es Salaam: Oxford University Press.

Walibora K. (2010). Uhalisia na Uhalisiamazingaombwe: Mshabaha kati ya Dunia Yao na The Tin Drum. Swahili Forum. 17 kur. 143-157.

Downloads

Published

30-09-2024

Issue

Section

Articles

How to Cite

Nafasi ya Wahusika Jumui katika Ujenzi wa Maudhui: Mifano kutoka Riwaya za Kimajaribio za Kiswahili. (2024). Mwanga Wa Lugha, 9(2), 25-35. https://journals.mu.ac.ke/index.php/mwl/article/view/529