Usawiri wa Nguvu-uhai katika Jamii za Kiafrika
Mifano Kutoka katika Riwaya ya "Mzishi wa Baba Ana Radhi"
Keywords:
Nguvu-uhai, Ontolojia ya KiafrikaAbstract
Nguvu-uhai ni kipengele muhimu katika falsafa ya maisha ya Waafrika na kitu muhimu kinachofanya tajiriba za Waafrika. Msukumo wa kuchunguza Nguvu-uhai katika jamii za Kiafrika kupitia riwaya ya Kiswahili unatokana na kuwapo kwa madai kuwa msingi wa jamii za Kiafrika kuamini kuwa viumbe vyote vina roho au uhai haukidhi kanuni za kimantiki na umepitwa na wakati (Smith, 1961). Hii ina maana kuwa Nguvu-uhai huchukuliwa kwa mitazamo tofauti kutegemeana na tajiriba na imani za kijamii. Kutokana na tofauti hizo za kimtazamo, tuliona ipo haja ya kuchunguza Nguvu-uhai katika jamii za Kiafrika ili kubainisha ujitokezaji wake katika riwaya za Kiswahili. Ili kutimiza azma hiyo ya utafiti huu riwaya ya Mzishi wa Baba Ana Radhi ilirejelewa. Data kutoka maktabani zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya usomaji makini na uhakiki wa riwaya teule. Uchambuzi wa data uliongozwa na Nadharia ya Ontolojia ya Kiafrika. Kwa kutumia mkabala wa kitaamuli data zilichambuliwa, zilichakatwa na kuwasilishwa. Matokeo yanaonesha kwamba Nguvu-uhai ni dhana pana katika jamii za Kiafrika na hugusa nyanja zote za maisha yao. Baadhi ya nyanja hizo ni kama vile na mila na desturi, maadili, afya ya jamii na uzazi. Kupitia vipengele hivyo maudhui mbalimbali kuhusu Waafrika huelezwa.