Uhifadhi wa Utamaduni Kupitia Mikakati ya Tafsiri

Mifano ya Riwaya za 'Kaburi bila Msalaba' na 'Bwana Myombekere na Bibi Bugonoka Ntulanalwo na Bulhawali'

Authors

  • Georginah Nyatichi Chuo Kikuu cha Moi Author
  • Mosol Kandagor Chuo Kikuu cha Moi Author
  • Nathan Ogechi Chuo Kikuu cha Kisii Author

Keywords:

Utamaduni, Tafsiri, Tasnia, Afrika

Abstract

Maendeleo katika tasnia ya tafsiri katika miaka ya awali, yalibadilisha mtazamo kuhusu dhana ya tafsiri na kutambua upana na mabadiliko yake. Kupanuka kwa taaluma ya tafsiri kumefanya mchakato wa tafsiri kujiegemeza zaidi kwa vipengele vya kitamaduni kuliko vipengele vya kiisimu. Katika mchakato wa tafsiri, maamuzi kuhusiana na uteuzi wa mbinu na mikakati ya kutafsiri yanaweza kushawishiwa na majukumu yanayokusudiwa kutekelezwa na tafsiri husika. Makala haya yanakusudia kueleza jinsi utamaduni wa kiafrika unadumishwa na kuhifadhiwa kupitia mikakati ya tafsiri katika matini teule za fasihi. Makala iljikita katika uchanganuzi wa tafsiri ya Kaburi Bila Msalaba (MC1) na Bwana Myombekere na Bibi Bugonoka Ntulanalwo na Bulhawali (MC2). Makala haya yalipania kutoa maelezo jinsi tafsiri ya riwaya za Kareithi na Kitereza ambazo ni hazina ya hifadhi ya utamaduni wa kijadi ya maisha ya kiafrika inavyochangia na kuendeleza uhifadhi wa utamaduni kutoka lugha moja hadi nyingine kupitia mikakati ya tafsiri. Data za makala haya zilikusanywa kwa kusoma na kuchambua matini chanzi Kaburi Bila Msalaba na Bwana Myombekere na Bibi Bugonoka Ntulanalwo na Bulhawali na matini lengwa, Unmarked Grave na Mr. Myombekere and His Wife Bugonoka, Their son Ntulanalwo and Daughter Bulihwali. Makala haya yalilenga kuangazia vipengele vya kitamaduni vilivyohawilishwa kutoka utamaduni chanzi na kuingizwa kwa utamaduni lengwa kwa kutumia mikakati maalum na jinsi vipengele hivi vilivyochangia uhifadhi wa utamaduni katika jamii mahususi. Mkabala wa kitaamuli ulitumika katika uwasilishaji wa data. Matokeo yalidhihirisha kwamba vipengele vya kitamaduni vimehawilishwa kutoka lugha moja kwenda nyingine kwa kutumia mikakati ya tafsiri. Hivyo basi, uhifadhi wa utamaduni katika matini teule umefanikishwa kupitia mikakati ya tafsiri.

References

Baker, M. (1992). In Other Words: A Coursebook on Translation. Routledge. London.

Fernandez, A. G. (2012). Translating Culture: Problems, Strategies and practical Realities. Retrieved form: file:/// c:/ Users/hp/Downloads/

Firoozkoohi, S. (2010). Culture Specific Items in Literary Translation. Translation Journal, 14(1), Oct. 2023. http://translationjournal.net/journal/51 culture. htm

Guerra, A. F. (2012). Translating Culture: Problems, Strategies, and Practical Realities. Journal of Literature Culture and Literary Translation, 1(3), 1–27.

Hervey, S., & H. I. (1992). Thinking Translation: A Course in Translation Method. London & New York: Routledge.

Kareithi, P. M. (2017). Unmarked Grave. Nairobi: Phoenix Publishers Ltd.

Kareithi, P. M. (1969). Kaburi Bila Msalaba. Nairobi: Phoenix Publishers.

Kitereza, A. (1981). Bwana Myombekere na Bibi Bugonoka na Ntulanalwo na Bulihwali. Dar es Salaam: Tanzania Publishing House.

Kitereza, A. (2002). Mr. Myombekere and His Wife Bugonoka, Their Son Ntulanalwo and Daughter Bulihwali. Dar es Salaam: Mkuki wa Nyota Publishers.

Leppihalme, R. (1997). Culture Bumps: An Empirical Approach to the Translation of Allusions. Clevedon: Multilingual Matters.

Mwansoko, H. (mh.). (2015). Kitangulizi cha Tafsiri: Nadharia na Mbinu. Toleo la Nne. Dar-es- Salaam: TUKI.

Newmark, P. (1988). Pragmatic Translation and Literalism. TTR: Traduction, Terminologie, Rédaction, 1(2), 133-145.

Nida, E. A. (1964). Language Structure and Translation, Stanford: Stanford University Press.

Pedersosen, J. (2005). How is Culture Rendered in Subtitles? Challenges in Multidimensional Translation. Proceedings of the Marie Curie Euroconferences Mu Tra: Saarbrucken, 2nd-6th May 2005. Stockholm Universitet 1-18.

Pembe, H. (2010). The Challenges of Translating Poetic Texts: The Case of Paul Sozingwa Wimbo wa Lawino. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Haijachapishwa.

Petrulione, L. (2012). Translation of Culture- Specific Items from English into Lithuanian: The Case of Joanne Harris’s Novel. Studies about Language no.21, 2012. Ktu. 43-49 http://www.kalbos.It/index/articleview/2305 (2023, OCT.13)

Pjuastuti, P. (2004). Students' Use of LI: A Study on Advanced Grammar Students’ Perspectives. (Doctoral Dissertation, Program Studi Pendidikan Bahasa Inggris FBS-UKSW).

Ruhumbika, G. (2002). Tafsiri za Fasihi za Kigeni katika Ukuzaji wa Fasihi ya Kiswahili. Fasihi III, Makala ya Semina za Kimataifa ya Waandishi wa Kiswahili. Dar-es-Salaam: TUKI.

Wafula, R. M. (2007). Review Essay and Book Reviews Review Essay: An Emic Reading of Drums of Death.

Downloads

Published

30-09-2024

Issue

Section

Articles

How to Cite

Uhifadhi wa Utamaduni Kupitia Mikakati ya Tafsiri: Mifano ya Riwaya za ’Kaburi bila Msalaba’ na ’Bwana Myombekere na Bibi Bugonoka Ntulanalwo na Bulhawali’. (2024). Mwanga Wa Lugha, 9(2), 13-24. https://journals.mu.ac.ke/index.php/mwl/article/view/527

Similar Articles

21-30 of 68

You may also start an advanced similarity search for this article.