Kiswahili kama Kichocheo cha Maendeleo ya Kiuchumi katika Nchi za Afrika Mashariki
Keywords:
Kiswahili, Kichocheo, Maendeleo, Kiuchumi, Afrika MasharikiAbstract
Kiswahili ni lugha ya matumizi mapana katika ukanda wa Afrika Mashariki. Katika juhudi ya kujiendeleza kiuchumi, jamii mbalimbali zinahitaji lugha ya mawasiliano ambayo inaeleweka kwa wahusika kama njia kuu ya kuafikia maendeleo. Aidha, kunahitajika juhudi za kimakusudi miongoni mwa wananchi za kuimarisha viwango vyao katika matumizi ya Kiswahili ili kuitumia lugha hiyo katika kushirikisha mipango anuwai ya kimaendeleo katika nyanja za kiuchumi. Ni kutokana na hali hii ambapo makala haya yanaonyesha mchango wa Kiswahili katika suala zima la maendeleo ya kiuchumi katika nchi za Afrika Mashariki. Data ya makala haya ilikusanywa kupitia kwa upekuzi wa maandishi yanayohusu mchango wa lugha katika maendeleo ya jamii pamoja na yale yanayohusu hali halisi ya maendeleo ya kiuchumi katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.