Ujitokezaji wa Viambishi vya Nafsi katika Kiarabu, Kitumbatu na Kiswahili

Authors

  • Sauda Uba Juma Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Author

Keywords:

Viambishi, Kategoria, Mapisi, Kusigana, Hayajatindimaa, Muasala

Abstract

Makala haya yanalenga kuchunguza ujitokezaji wa viambishi vya nafsi katika Kiarabu Kitumbatu na kuvilinganisha na Kiswahili. Lengo la uchunguzi huo ni kutaka kubaini jinsi vipengele hivyo vinavyoingiliana na kusigana. Hii inatokana na ukweli kwamba mapisi ya lugha ya Kiswahili na lahaja zake pamoja na lugha ya Kiarabu mpaka sasa hayajatindimaa kwa kuwa lugha hizi zilikuwa na mtagusano na muasala wa muda mrefu tangu 800 BK. Kutokana na hali hiyo kumeibuka mitazamo kinzani juu ya uhusiano wa Kiswahili na Kiarabu. Kuwepo kwa baadhi ya maneno ya Kiarabu katika Kiswahili kumechochea hoja kwamba Kiswahili kinatokana na Kiarabu. Mjadala huo ni wa muda mrefu ambao unaendelea hadi sasa. Baadhi ya tafiti tangulizi zimebainisha idadi kubwa ya maneno ya Kiswahili yenye asili ya Kiarabu. Hata hivyo, mfanano huo wa kimsamiati baina ya Kiswahili na Kiarabu haujitoshelezi kutoa hitimisho juu ya chimbuko la Kiswahili. Baadhi ya watafiti waliochunguza maneno ya Kiarabu katika Kiswahili wamebaini kuwapo kwa asilimia kubwa ya mfanano wa kategoria ya nomino baina ya lugha hizi mbili kuliko katika kategoria zingine. Hivyo pamoja na kuwepo kwa kategoria mbalimbali za maneno, utafiti huu umejibana kushughulikia jinsi viambishi vya nafsi vinavyojitokeza katika kategoria ya vitenzi vya Kiarabu, Kitumbatu na kuvilinganisha na Kiswahili. Hii ni kwa sababu kwa kuwa imeshatibitika kwamba, Kitumbatu ni miongoni mwa lahaja ya Kiswhili, ujitokezaji huo wa viambishi utatupa mwanga kati ya uhusiano wa Kiarabu na Kiswahili. Chanzo ya data za utafiti huu zimekusanywa kupitia usomaji wa nyaraka, vitabu na kamusi mbalimbali zilizoandikwa kuhusu kategoria hiyo. Vilevile, tulipitia nyaraka hizo ili kupata maarifa ya jumla kuhusu ujitokezaji wa viambishi vya nafsi kwa mujibu wa waandishi mbalimbali. Data zingine zilikusanywa uwandani kupitia mbinu ya usaili na hojaji kwa wazungumzaji wa Kiarabu na Kitumbatu. Aidha utafiti huu umeongozwa na Nadharia ya Fonolojia Umbo Upeo kuanzia sasa (UU). Kwa ujumla matokeo ya utafiti huu yameonesha kwamba Kitumbatu kina uhusiano zaidi na Kiswahili kuliko Kiarabu. Hii ni kudhihirisha kwamba Kiswahili na Kiarabu ni lugha mbili ambazo hazina uhusiano wa kimnasaba kwa kuwa hazikuchipukia kutoka kwenye lugha yenye asili moja.

References

Aghel, A. M. (2021). Ulinganishi wa Mofolojia ya Vitenzi vya Kiswahili na Kiarabu. Tasnifu ya Uzamivu [Haijachapishwa]. Chuo Kikuuu Huria cha Tanzania.

BAKIZA (2010). Kamusi la Kiswahili Fasaha. Oxford University Press.

Chomi, E. W. (2013). Kitangulizi cha Mofolojia ya Kiswahili. TUKI.

Chomi, E. W. (2013). Muundo wa Viambajengo vya Sentensi za Kiswahili. TUKI. Z

Dawson, C. (2007). A Practical Guide to Research Methods. How to Book Limited.

Habwe, J. na Karanja, P. (2012). Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Phoenix Publishers.

Juma, H. K. (2019). Ulinganishi wa Kihistoria na Kiisimu wa Lahaja za Kiamu, Kimvita, Kipemba, Kitumbatu na Kimakunduchi. Tasnifu ya Uzamivu [Haijachapishwa]. Chuo Kikuuu cha Dar es Salaam.

Khamis, A. B na Kiango, G. C. (2002). Uchanganzi wa Sarufi ya Kiswhili. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Kihore, Y. M. na wenzake (2003). Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu (SAMAKISA): Sekondari na Vyuo. TUKI.

Masebo, J. A. & Nyangwine, N. (2006). Nadharia ya Lugha: Kiswahili 1. Nyambari Nyangwine Publishers

Massamba, D. P. B. (2004). Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha. TUKI.

Massamba, D. P. B. (2017). Historia ya Kiswahili. Mtazamo Mpya 100KK Hadi 2000BK. Kiswahili Development Ltd.

Matinde, R. S. (2012). Dafina ya Lugha Isimu na Nadharia; Kwa Sekondari, Vyuo Vikuu vya Kati na Vyuo Vikuu. Serengeti Educational Publishers (T) Ltd.

McCarthy, J. & Prince A. (1993). Prosodic Morphology 1: Constrain Interaction and Satisfaction. In Technical report No. 3 Amherst. University of Massachusetts and new Brunswick N. J Rutgers University.

McCarthy, J. & Prince, A. (1993). Prosodic Morphology 1: Constrain Interaction and Satisfaction. In Technical report No. 3 Amherst. University of Massachusetts and New Brunswick N. J Rutgers University.

Mgullu, R. S. (1999). Mtaala wa Isimu: Fonetiki, Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahii. Longhon Publishers.

Ponera, A. S. (2019). Misingi ya Utafiti wa Kitaamuli na Uandishi wa Tasnifu. Central Tanganyika Press.

Prince, A. & Smolensky, P. (1993). Optimality Theory: Constraint Interaction in Generative Grammar. Oxford.

Rubanza, Y. I. (1996). Mofolojia ya Kiswahili. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Rubanza, Y. I. (2003). Sarufi Mtazanmo wa Kimuundo. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

TUKI (1990). Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Downloads

Published

30-09-2024

Issue

Section

Articles

How to Cite

Ujitokezaji wa Viambishi vya Nafsi katika Kiarabu, Kitumbatu na Kiswahili. (2024). Mwanga Wa Lugha, 9(2), 1-12. https://journals.mu.ac.ke/index.php/mwl/article/view/526