Uundaji wa Lakabu za EkeGusii
Keywords:
Lakabu, Uundaji, EkeGusii, UambatanishajiAbstract
Lakabu hutumika kila mara katika jamii kuwarejelea watu wa kila tabaka. Kila mtu anaweza kujipa lakabu au akapatiwa jina hilo na wanajamii bila kujali iwapo atalipenda jina hilo au la. Makala haya yanafafanua mbinu mbalimbali za lugha zinazotumiwa katika kuunda lakabu za wachezaji kandanda katika kaunti dogo ya Kenyenya; kaunti ya Kisii; Kenya. Watafitiwa walikuwa baadhi ya wachezaji wa kandanda na pia mashabiki sugu wa mchezo huu waliochaguliwa kimakusudi. Data ya kimsingi ilikusanywa nyanjani kupitia mahojiano ya moja kwa moja. Mahojiano haya yaliongozwa na maswali teule yaliyolenga kuibua hisia lengwa. Data nyingine ilikusanywa makitabani kutokana na kazi teule. Matokeo ya utafiti huu yalidhihirisha kuwa lakabu uundwa kwa kutumia mbinu mbalimbali kama vile: kuambisha au kudondosa viambishi vya nomino mbalimbali, kuunganisha nomino mbili, kutoka kwa nomino za pekee kama majina halisi ya watu, kutokana na vitenzi, vivumishi na vielezi. Pia kuna baadhi ya lakabu zinazoundwa kutokana na mbinu ya utohozi, ukopaji, ufupishaji wa maneno, uambatanishaji na pia uhamishaji wa maana kama inavyodhihirika katika makala haya.