Mikabala ya Uchanganuzi wa Hiponimia na Uainishaji Wake

Authors

  • Benard Odoyo Okal Chuo Kikuu cha Maseno Author

Keywords:

Hiponimia, Fahiwa, Mkabala, Taksonimia

Abstract

Wataalamu mbalimbali wa Kiswahili wameshughulikia tafiti za hiponimia ya kategoria za nomino na vitenzi huku wakitoa mifano anuwai. Hata hivyo, tafiti hizo hazijadhihirisha mikabala inayoweza kutumiwa kuichanganua kama vile mkabala wa kisayansi na kiisimu. Vilevile hakuna mitindo ya uainishaji wa hiponimia ambayo imewahi kuangaziwa katika Kiswahili mbali na kutajataja tu hipanimu husika na zile hiponimu zake. Hivyo basi, makala hii imeshughulikia mikabala ya uchanganuzi wa hiponimia na uainishaji wake kwa kulenga leksimu za Kiswahili hasa za kategoria za nomino na vitenzi zilizoteuliwa kidhamirifu kutoka kamusi anuwai za Kiswahili. Makala hii imedhihirisha kuwa hiponimia inaweza kuchanganuliwa kwa kuzingatia mikabala miwili: mkabala wa kisayansi na kiisimu. Aidha, uainishaji wa hiponimia za kategoria za nomino na vitenzi huweza kufanywa kwa kuzingatia mkabala wa kiisimu katika misingi sita maalum kama vile: kitambuzi, kiuamilifu, kijiografia, kitukio, kihali na kitendo.

Downloads

Published

01-09-2020

Issue

Section

Articles