Matumizi ya Kiswahili katika Bidhaa za Watoto Nchi Tanzania
Yaliyomo na Yasiyokuwamo
Keywords:
Kiswahili, Bidhaa, Watoto, TanzaniaAbstract
Makala haya ni sehemu ya utafiti uliofanyika katika Jiji la Dodoma. Utafiti uliongozwa na malengo makuu matatu. Mosi, kubainisha bidhaa za watoto na kutoa tathmini ya jumla kuhusu hali ilivyo katika matumizi ya lugha ya Kiswahili. Pili, kuonesha lugha zinazotumika katika bidhaa za watoto. Tatu, kujadili umuhimu wa matumizi ya lugha ya Kiswahili katika bidhaa za watoto. Mbinu zilizotumika katika ukusanyaji data ni udurusu wa kimaktaba na ushuhudiaji. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa Kiswahili hakijatumika kwa kiasi kikubwa katika bidhaa za watoto. Lugha za Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu, Kichina na Kituruki zimeonekana kutawala katika bidhaa za watoto nchi Tanzania. Hali hii inakidunisha Kiswahili na kuzipa hadhi kubwa lugha za nje. Aidha, kwa upande wa walaji/watumiaji wa bidhaa, matumizi ya lugha za kigeni yanaweza kuwa hatari kiusalama kwa kuwa, wanatumia bidhaa ambazo hawajui matumizi yake kiusahihi.