Changamoto katika Kutathmini Stadi za Kusikiliza na Kuzungumza katika Kiswahili kwenye Mitihani ya KCPE na KCSE nchini Kenya

Authors

  • Mary N. Ndung’u Chuo Kikuu cha Nairobi Author

Keywords:

Tathmini, Tathmini Endelevu, Tathmini Tamati, Upimaji, Ujuzi, Uchanganuzi Matini

Abstract

Tathmini ya ujuzi wa wanafunzi katika elimu ina nafasi kubwa kwa sababu huwa na malengo kama vile kutafuta thamani au ubora wa madhumuni ya masomo yanayowekwa na mwalimu, mbinu za kufundisha na hata thamani ya maarifa yanayopitishwa kwa wanafunzi. Vipengele vya lugha ambavyo huhitaji kutathminiwa kila wakati kupitia tathmini endelevu au baada ya kipindi fulani cha wakati kupitia tathmini tamati ni stadi za kusikiliza, kuzungumza, kuandika, na kusoma. Ikiwa hizi ndizo aina za tathmini maarufu katika kupima viwango mbalimbali vya maarifa, basi pana haja ya kuchunguza jinsi tathmini hizi hususan tathmini tamati katika mitihani ya KCPE na KCSE nchini Kenya inavyofanikisha kupima ujuzi wa wanafunzi katika stadi za kusikiliza na kuzungumza katika lugha ya Kiswahili. Katika kufanya hivyo, makala haya yanaangazia mbinu zinazotumiwa na changamoto wanazokumbana nazo Baraza la Mitihani la Taifa Nchini Kenya (Kenya National Examination Council, KNEC) katika kuandaa tathmini za stadi za lugha hususan kusikiliza na kuzungumza. Aidha, pana haja ya kutoa mapendekezo ya jinsi ya kukabiliana na changamoto hizo. Mtazamo wa Uchanganuzi Matini (Frey, 1999) unatumiwa kuelekeza uchunguzi katika makala haya.

Downloads

Published

30-04-2021

Issue

Section

Articles