Changamoto za Kuunda Programu Tumizi ya 'Kikagua-Tahajia' ya Lugha za “Runyačitara”

Authors

  • Caroline Asiimwe Chuo Kikuu cha Makerere Author

Keywords:

'Kikagua-Tahajia', Changamoto, Maneno Mnasaba, Mofofonolojia, Othografia, “Runyačitara”

Abstract

Makala haya yanafafanua changamaoto za kuunda programu tumizi ya kikagua-tahajia cha lugha za “Runyačitara”. Kwa kuwa lugha za “Runyačitara” ni lugha ambishi bainishi, maumbo ya maneno na uchanganuzi wake kimofolojia ni changamani. Uchangamani huu unafafanuliwa na namna unavyozua changamoto za kiothografia, kimofolojia na kileksika katika mchakato wa kuandaa kikagua-tahajia. Data kutoka uwandani na maktabani imechambuliwa kwa kutumia mbinu linganishi. Imebainika kwamba ili maneno yaweze kutumiwa katika mchakato wa kukagua-tahajia, kuna haja ya kuunda kamusi ya leksimu ambayo itaingizwa kweye kompyuta, kuelezea othografia, ruwaza na kanuni za undaji wa maneno na sarufi maumbo ya lugha za “Runyačitara” kwa ujumla. Katika kufanya hivyo, makala haya yanabaini kwamba ingawa kuna maneno mnasaba, kuna changamoto za kimofofonolojia na za kileksika katika maneno ya lugha hizi. Kwa miundo inayofanana kanuni za kuandaa maneno kwa ajili ya kikagua- tahajia zimependekezwa.

Downloads

Published

30-06-2019

Issue

Section

Articles

How to Cite

Changamoto za Kuunda Programu Tumizi ya ’Kikagua-Tahajia’ ya Lugha za “Runyačitara”. (2019). Mwanga Wa Lugha, 3(Toleo Maalum), 207-222. https://journals.mu.ac.ke/index.php/mwl/article/view/145

Similar Articles

11-20 of 54

You may also start an advanced similarity search for this article.