Motifu ya Safari katika Kazi za M. S. Mohammed

Authors

  • Evans Mbuthia Chuo Kikuu cha Nairobi Author

Keywords:

Motifu, Sosholojia ya Kifasihi, Saikolojia, Hisia, Kutamauka, Mwamko

Abstract

S. Mohammed ni mwandishi maarufu katika fasihi ya Kiswahili. Kazi zake tatu ambazo zinamulikwa katika makala haya zinamtambulisha kama mwandishi ambaye ana mazoea ya kutumia mbinu ya safari ili kukuza maudhui yake. Wahusika wake wanapitia tajriba anuwai katika safari zao ambazo zinawapelekea kukua, kujitambua, kujinasua, kukengeuka na hata kuangamia. Katika kazi zake zilizoteuliwa: Kiu, Nyota ya Rehema na Kicheko cha Ushindi. Hali hizi zinajitokeza na kuwa kama funzo kwa wasomaji ambao wanashauriwa kuzingatia waendako na waendavyo. Ni bayana kwamba motifu ya safari ina nafasi muhimu katika kazi za M. S. Mohammed na makala haya yanazamia hilo suala kwa kina. Ili kuweka mambo bayana, makala haya yametumia Sosholojia ya Kifasihi kama kurunzi ya kumulika wanayoyapitia wahusika katika kazi zilizoteuliwa.

Downloads

Published

30-06-2019

Issue

Section

Articles

How to Cite

Motifu ya Safari katika Kazi za M. S. Mohammed. (2019). Mwanga Wa Lugha, 3(Toleo Maalum), 61-70. https://journals.mu.ac.ke/index.php/mwl/article/view/136

Similar Articles

21-30 of 181

You may also start an advanced similarity search for this article.