Uchanganuzi wa Muziki Uliopendwa na Muziki wa Kisasa
Keywords:
Muziki, uliopendwa, kisasa, jamiiAbstract
Muziki ni mojawapo ya vipera muhimu vya fasihi simulizi. Jumbe muhimu kuhusu masuala mbalimbali yanayoathiri jamii huwasilishwa kupitia muziki. Aidha, muziki umeweza kutumika kutoa habari kuhusu mambo ambayo huchukuliwa mwiko na, kwa hivyo, hayawezi kujadiliwa katika vikao na mazungumzo ya kawaida. Baadhi ya sifa za muziki zinazoufanya kutumika kwa urahisi ni pamoja na matumizi ya tamathali za usemi (kama vile mafumbo, methali na tashbihi) midundo na matumizi ya mahadhi yanayotokana na ala zinazotumika katika muziki. Makala haya yananuia kulinganisha muziki uliopendwa na muziki wa kisasa. Ulinganishi utahusu matumizi ya mapambo ya lugha kama vile tamathali za usemi, methali, semi na mafumbo katika aina hizo mbili za muziki kwa lengo la kuonesha ni muziki upi ulio na matumizi pevu ya lugha na hivyo unaoweza kutumika katika kuendeleza lugha ya Kiswahili. Muziki wa bendi ya DDC Mlimani Park utatathminiwa kwa kuzingatia kategoria ya muziki ulioopedwa na ule wa bendi ya Sauti Sol katika kategoria ya muziki wa kisasa.Downloads
Published
30-04-2019
Issue
Section
Articles
How to Cite
Uchanganuzi wa Muziki Uliopendwa na Muziki wa Kisasa. (2019). Mwanga Wa Lugha, 3(1), 63-74. https://journals.mu.ac.ke/index.php/mwl/article/view/111