Changamoto katika Kutafsiri Matini za Kisayansi
Keywords:
Changamoto, Matini za KisayansiAbstract
Makala haya yanajadili kuhusu changamoto zinazojitokeza wakati wa kutafsiri matini za kisayansi na mbinu za kukabiliana na changamoto hizo. Tafsiri ya matini za kisayansi, kwa mujibu wa Ghazala (1995), inahusu kufasiri maneno, hasa katika uga wa sayansi na tekinolojia wa aina zote, kutoka lugha moja kwenda lugha nyingine. Kutokana na maendeleo ya sayansi na tekinolojia, ni dhahiri kwamba tafsiri katika uga huu haiwezi kuepukika. Hata hivyo, kwa mujibu wa Mwansoko na wenzake (2006), tafsiri ya kisayansi ni miongoni mwa tafsiri ngumu kulinganisha na tafsiri nyingine. Kwa hivyo, makala haya yamechunguza changamoto zinazosababisha ugumu huo na namna ya kukabiliana nao. Data za utafiti zimepatikana kwa njia ya dodoso na kuchanganuliwa kwa kuongozwa na Nadharia ya Aina ya Matini iliyoasisiwa na Reiss miaka ya 1970. Aidha, matokeo ya utafiti yamebaini kwamba changamoto za kutafsiri matini za kisayansi zinasababishwa na mambo yafuatayo: uvumbuzi wa kisayansi, ugumu wa istilahi katika matini za kisayansi, kukosekana kwa visawe vya moja kwa moja katika lugha lengwa, uchache wa vifaa na ukubwa wa gharama za vifaa vya tafsiri na mfumuko wa istilahi mbalimbali zinazorejelea dhana moja. Kadhalika, utafiti umebaini kwamba zipo mbinu zinazoweza kutumika kukabiliana na changamoto hizo kama vile; uundaji wa maneno mapya, ufafanuzi, kununua vifaa bora vya tafsiri na wataalamu kukubaliana na kuchagua istilahi zinazofaa zaidi.
References
Abdalla, S. A. (2016). Changamoto za Kutumia Istilahi Mbili kwa Dhana Moja katika Kufundisha Isimu na Fasihi Shule za Sekondari: Mifano kutoka Mkoa wa Kusini-Pemba, Tanzania [Tasnifu ya Umahiri]. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Tanzania.
Al-Abbas, L. S., & Haider, A. S. (2021). Using Modern Standard Arabic in Subtitling Egyptian Comedy Movies for the Deaf/Hard of Hearing. Cogent Arts & Humanities, 8(1).
Al-Hassnawi, A. R. A. (2010). Aspects of Scientific Translation: English into Arabic Translation as a Case Study. Retrieved from http://www.translationdirectory.com/article10.htm
Al-Smadi, H. M. (2022). Challenges in Translating Scientific Texts: Problems and Reasons. Journal of Language Teaching and Research, 13(3), 550-560.
Byrne, J. (2006). Technical Translation: Usability Strategies for Translating Technical Documentation. Dordrecht: Springer.
Costales, A. F. (2011). Translation 2.0: Facing the Challenge of Global Era. Linguistica Antverpiesia (Toleo Jipya), 179-194.
Ghazala, H. (1995). Translation as Problems and Solutions. Valita: LGA Publication.
Kingscott, G. (2002). Technical Translation and Related Disciplines: Perspectives. Studies in Translatology, 10(4), 247-255.
Malangwa, P. S. (2017). Mchango, Maendeleo na Changamoto Zinazokabili Taaluma za Tafsiri na Ukalimani katika Kiswahili. Eldoret: Moi University Press.
Mahero, T., & Kandagor, M. (2020). Changamoto za Tafsiri katika Enzi ya Utandawazi. MULIKA, 39, 159-168.
Munday, J. (2012). Introducing Translation Studies: Theories and Applications (3rd Ed.). London and New York: Routledge.
Mwansoko, H. J. M, Mekacha R. D. K., Masoko, D. L. W., & Mtesigwa, P. C. K. (2006). Kitangulizi cha Tafsiri: Nadharia na Mbinu. Dar es Salaam: TUKI.
Nida, E. A. (1964). Towards a Science of Transilating with Special Reference to Principles and Procedures Involved in Bible Translating. Leiden: Brill.
Nida, E. A., & Taber, C. R. (1969). The Theory and Practice of Translation. London: Prentice Hall.
Okot, P. B. (1975). Wimbo wa Lawino (Translation of Song of Lawino). Nairobi: East African Educational Publishing House.
Shakespeare, W. (1969). Juliasi Kaizari (Translation of Julius Caesar). Dar es Salaam: Oxford University Press.
Shakespeare, W. (1969). Mabepari wa Venisi (Translation of Merchants of Venice). Dar es Salaam: Oxford University Press.
Shiyab, S .M., Rose, M. G., House, J., & Duval, J. (2010). Globalization and its Impact on Translation. UK: Cambridge Scholar Publishing Print.
Sieny, M. E. (1985). Scientific Terminology in the Arab world: Production, Co-ordination, and Dissemination. Meta: Journal des Traducteurs/Meta: Translators' Journal, 30(2), 155-160.
Thiongo, N., & Minii, N. (1982). Nitaolewa Nikipenda (Translation of I will Mary when I Want). East Africa Educational.
TUKI. (2004). Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Nairobi: Oxford University Press.