Athari ya Mielekeo ya Walimu wa Shule za Msingi kuhusu Ufundishaji wa Kiswahili na Mazoezi Yake katika Mtaala wa Umilisi

Authors

  • Nyandwaro K. Lena Chuo Kikuu cha Rongo Author
  • James O. Ontieri Chuo Kikuu cha Rongo Author
  • Sangai Mohochi Chuo Kikuu cha Kibabii Author

Keywords:

Mielekeo, Walimu, Kiswahili, Umilisi, Athari

Abstract

Tafiti nyingi zimeonyesha kuwa mielekeo ya walimu huwa na athari miongoni mwa wanafunzi. Sababu ni kuwa wanatangana nao kwa asilimia kubwa ya muda. Makala haya yanajadili athari ya mielekeo ya walimu kuhusu ufundishaji wa Kiswahili na mazoezi yake katika Mtaala wa Umilisi kwa kujikita kwenye Gatuzi dogo la Masaba Kusini. Mtaala wa Umilisi umechukua nafasi ya Mtaala wa 8-4-4 ambao umekuwa ukitumika nchini Kenya kwa zaidi ya miongo mitatu. Mtaala wa Umilisi kwani unasisitiza utendaji wa yale mwanafunzi amefundishwa ili kuboresha umilisi wake na kuwa na ujuzi wa kutumia maarifa aliyopata katika maisha yake ya kila siku. Makala haya yanatalii namna mielekeo ya walimu kuhusu ufundishaji wa Kiswahili imeweza kuathiri wanafunzi. Nadharia ya Vitendo Vilivyofikiriwa ilizingatiwa katika makala haya. Data ilikusanywa miongoni mwa wasailiwa kwa kutumia mijadala ya makundi madogo ya wanafunzi kumi kutoka gredi ya kwanza hadi tatu kutoka shule kumi ambazo ziliteuliwa kimaksudi. Pia, wasailiwa waliteuliwa kimaksudi. Waliulizwa maswali na majibu yalinakiliwa na kurekodiwa na mtafiti akisaidiwa na walimu wao kwa sababu walikuwa wachanga. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa na kuwasilishwa kupitia majedwali ambayo yalijadiliwa kwa kina. Makala haya ni muhimu kwani itawasaidia walimu kujua zaidi athari waliyo nayo kwa wanafunzi na itasaidia katika kuboresha utekelezaji wa kina na ufundishaji bora wa Kiswahili katika Mtaala wa Umilisi.

References

Ajzen, I., na Fishbein, M. (2020). Understanding Attitudes and Predicting Social Behaviour. Eaglewood Cliffs, NJ: Prentice-Hall.

Codina, N., Valenzuela, R., Pestana, J. V., na Gonzalez-Conde, J. (2018). Relations between Student Procrastination and Teaching Styles: Autonomy, Supportive and Controlling. Psychology. 9, 809. doi: 10.3389/fpsyg.2018.00809.

Fraser, L. E. (2014). Teacher Efficacy Beliefs: How General Teachers Feel towards English Language Learners. Capstones paper 828. Uk. 1-56.

Granaos, F. C. na wenzake. (2020). A Descriptive Study on the Training and Attitude of Future Teachers towards Educational Inclusion. Sustainability, 12(19), 1-14.

Hamer, L. na Keefe, R. (2013). Achieving Change in Students’ Attitude towards Group Projects by Teaching Group Skills. Journal of Higher Education Theory and Practice, 25-33. https://via.library.depaul.edu/buspubs/71.

Karabenick, S. A. na Noda, P. A. C. (2004). Professional Development Implications of Teachers' Beliefs and Attitudes toward English Language Learners. Biling. Res. J., 28(1), 55-75.

Liu, L. na Jackson, J. (2019). Building Learner Self Belief in Oral Communique via Remarks. Journal of Language Teaching and Research, 10(3), 647-660.

Pryor, N. J. na Johnson, C. C. (2018). Assessing the Impact of Instructors’ Terrible Mindset on Pupil Fulfilment. Teachers College Record, 120(10), 1-40.

Simala, I. K. (2016). Fasihi Ibuka ya Kiswahili. Hli na Mustakabali Wake. Katika Mwita, L. C. (Mh.), Kiswahili na Utandaazi (116-136). Nairobi: Twaweza Comunications.

Sugano, S. G. C. na Mamolo, L. A. (2021). The Effects of Teaching Methodologies on Students’ Attitude and Motivation. Meta-analysis. Int. J. Instr, 14, 827–846. doi: 10.29333/iji.2021.14348a.

Taasisi ya Elimu ya Kenya (2006). Kiswahili Sekodari: Mwongozo wa Mwalimu. Nairobi: Taasisi ya Elimu.

Takase, M., Niitani, M., Imai, T. na Okada, M. (2019). Students’ Perceptions of Teaching Factors that Demotivate their Learning in Lectures and Laboratory-Based Skills Practice. Int. J. Nurs. Sci., 6, 414–420. doi: 10.1016/j.ijnss.2019.08.001.

Ulug, M., Odzen, S. M. na Eryilmaz, A. (2011). The Effects of Teachers' Attitudes on Students' Personality and Performance. Proc. Soc. Behav. Sci., 30, 738-742.

Walsh, P., Owen, P. A. Mustafa, N. na Beech, R. (2020). Learning and Teaching Approaches Promoting Resilience in Student Nurses: An Integrated Review of the Literature. Nurse Educational. Practicet, 45, 8. doi: 10.1016/j.nepr.2020.102748.

Yadav, M., na Baniata, H. (2013). Factorizing Demotivation, Findingmotivation: A Constructive Approach to Quality Enhancement. Procedia Soc. Behav. Sci., 70,120–130. doi: 10.1016/j.sbspro.2013.01.047.

Zang, Y. na Li, Y. (2018). The Impact of Instructors’ Negative Attitude Closer to Secomd Language Errors on College Students’ Anxiety aad Willingness to Communicate in English. Journal of Teaching and Research, 9(5), 948-956.

Downloads

Published

30-04-2025

Issue

Section

Articles

How to Cite

Athari ya Mielekeo ya Walimu wa Shule za Msingi kuhusu Ufundishaji wa Kiswahili na Mazoezi Yake katika Mtaala wa Umilisi. (2025). Mwanga Wa Lugha, 10(1), 1-10. https://journals.mu.ac.ke/index.php/mwl/article/view/539

Similar Articles

11-20 of 180

You may also start an advanced similarity search for this article.