Nafasi ya Nyimbo za Kizazi Kipya katika Kufundishia Masuala Mtambuko katika Mtaala wa Umilisi

Authors

  • Nyandwaro K. Lena Chuo Kikuu cha Rongo Author
  • Alfred Malugu Chuo Kikuu cha Rongo Author

Keywords:

Mtaala wa Umilisi, Masuala Mtambuko, Nyimbo za Kizazi Kipya

Abstract

Hitaji mojawapo katika Mtaala wa Umilisi nchini Kenya ni kuwa wanafunzi wanapaswa kufundishwa masuala mtambuko. Lengo la kuwafundisha masuala mtambuko ni kuwasaidia wawe wabunifu na wapate ujuzi wa kukabiliana na masuala haya katika mazingira yao ya kila siku. Mtaala huu unasisitiza kuwa mwalimu anapaswa kuwa mbunifu katika ufundishaji wake ili kukuza umilisi wa wanafunzi. Njia mojawapo ya kufundisha masuala kiubunifu ni kupitia matumizi ya nyimbo za kizazi kipya ambazo zina maudhui ya masuala mtambuko mbalimbali. Nyimbo hizi zinapendwa na vijana ambao hujihusisha nazo na wao huzisikiliza kupitia vyombo mbalimbali vya habari. Makala haya yanachanganua baadhi ya nyimbo za kizazi kipya na jinsi mwalimu anavyoweza kuzitumia kufundishia masuala mtambuko darasani ili kufikia malengo yake na matarajio ya jamii kwa ujumla. Nadharia iliyoongoza makala haya ni Nadharia ya Utekelezaji wa Mtaala iliyoasisiwa na Gross (1971).

Downloads

Published

30-04-2024

Issue

Section

Articles