Kufifia kwa Lahaja za Kiswahili katika Karne ya 21

Mfano wa Lahaja ya Kimakunduchi

Authors

  • Zainab Ali Iddi Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Author

Keywords:

Lahaja, Kiswahili, Karne ya 21, Kimakunduchi, Elimu, Utamaduni, Teknolojia

Abstract

Makala haya yanachunguza mambo yanayochangia kufifia kwa lahaja za Kiswahili katika karne ya 21 kwa kutumia lahaja ya Kimakunduchi ya Kusini Unguja, kama mfano mahsusi. Lahaja hii, mojawapo ya lahaja kongwe za Kiswahili, imekuwa sehemu muhimu ya utambulisho, urithi na historia ya jamii ya Wamakunduchi. Lakini kwa sasa inakabiliwa na tishio kubwa la kupotea kutokana na sababu mbalimbali za kijamii, kiuchumi, kiteknolojia na kisera. Hoja kuu za makala zinajikita katika athari za upendeleo wa Kiswahili Sanifu katika mifumo rasmi kama vile elimu, utawala na vyombo vya habari, hali inayosababisha jamii kuitazama lahaja yao kama lugha duni au isiyo rasmi. Aidha, makala imeeleza namna mabadiliko ya kijamii na kiuchumi, ikiwemo uhamiaji, ndoa mseto na maendeleo ya kiteknolojia, vinavyochangia vijana kuachana na matumizi ya Kimakunduchi katika mazingira ya nyumbani na kijamii. Aidha, makala imejikita katika uchambuzi wa kina kwa kutumia Nadharia ya Ikolojia ya Lugha ya Haugen (1972), ambayo inafafanua mahusiano baina ya mazingira ya kijamii na ustawi au kufifia kwa lahaja. Pia, taarifa kutoka tafiti ndogo zilizofanyika Zanzibar zinathibitisha mwenendo wa kupungua kwa idadi ya wazungumzaji vijana wa Kimakunduchi, jambo linalodhihirisha hali mbaya ya lahaja hiyo. Makala inapendekeza hatua za kuchukuliwa ili kuhifadhi na kuhuisha lahaja ya Kimakunduchi, ikiwemo kuweka sera madhubuti za elimu na utamaduni, kutumia teknolojia katika kuandaa maandiko na rekodi za lahaja, pamoja na kushirikisha jamii na wazee wenye ufasaha katika ufundishaji na uhamasishaji wa matumizi ya lahaja hiyo kama sehemu muhimu ya urithi na utambulisho wa Zanzibar.

References

Batibo, H. M. (2005). Language decline and death in Africa: Causes, consequences and challenges. Multilingual Matters.

Crystal, D. (2008). Language death. Cambridge University Press.

Fishman, J. A. (1991). Reversing language shift: Theoretical and empirical foundations of assistance to threatened languages. Multilingual Matters.

Haugen, E. (1972). The ecology of language. Stanford University Press.

Iddi, Z.A. (2011). Phonological Processes in Kimakunduchi Dialect. Tasnifu ya Shahada ya Umahiri (haijachapishwa). Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Iddi, Z.A. (2018). Ulinganishi wa Kiisimu wa Kitumbatu na Kimakunduchi. Tasnifu ya Shahada ya Uzamivu (haijachapishwa). Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar.

Juma, H.K. (2019). Ulinganishi wa Kihistoria na Kiisimu wa Lahaja za Kiamu, Kimvita, Kipemba, Kitumbatu na Kimakunduchi. Tasnifu ya Shahada ya Uzamivu (haijachapishwa). Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Massamba, D.P.B. (2017). Historia ya Kiswahili: Mtazamo Mpya. Kiswahili Development Limited.

Mazrui, A. M. & Mazrui, A. A. (1995). Swahili state and society: The political economy of an African language. East African Educational Publishers.

Mdee, J. S. (2010). Fasihi simulizi na uhifadhi wa lugha za Kiafrika. TUKI Working Papers, University of Dar es Salaam.

Mulokozi, M. M. (2002). Development of Kiswahili as a national and official language: The case of Tanzania. In Language and Development in Africa.

Nurse, D. & Hinnebusch, T. J. (1993). Swahili and Sabaki: A linguistic history. University of California Press.

Qorro, M. A. S. (2009). Parents’ and policy makers’ insistence on foreign languages as media of education in Africa: Restricting access to quality education – for whose benefit? In B. Brock-Utne & I. Skattum (Eds.), Languages and education in Africa: A comparative and transdisciplinary analysis (pp. 31–48). Symposium Books.

UNESCO. (2003). Language vitality and endangerment. UNESCO Ad Hoc Expert Group on Endangered Languages.

Downloads

Published

30-09-2024

Issue

Section

Articles

How to Cite

Kufifia kwa Lahaja za Kiswahili katika Karne ya 21: Mfano wa Lahaja ya Kimakunduchi. (2024). Mwanga Wa Lugha, 9(2), 111-122. https://journals.mu.ac.ke/index.php/mwl/article/view/537

Similar Articles

1-10 of 235

You may also start an advanced similarity search for this article.