Usawiri wa Mwanamke katika Nyimbo za Sifo za Wakamba

Authors

  • Dorcas Kasiva Kimondiu Chuo Kikuu cha Machakos Author
  • Larry Ndivo Chuo Kikuu cha Machakos Author
  • Vifu Saidi Makoti Chuo Kikuu cha Machakos Author

Keywords:

Usawiri, Nyimbo, Sifo, Wakamba

Abstract

Makala haya yanachambua usawiri wa mwanamke katika baadhi ya nyimbo za sifo za Wakamba nchini Kenya. Ili kufafanua namna mwanamke alivyosawiriwa na wasanii wa nyimbo hizi za sifo za Wakamba, tutawarejalea wasanii wachache wa nyimbo za sifo za Wakamba. Makala hii inaegemea  nadharia ya Ufeministi wa Kiafrika. Nadharia hii imetumika kuongoza uchunguzi wa jinsi mwanamke Mwafrika  alivyosawiriwa na watunzi hawa wa nyimbo za sifo za Wakamba ambao ni watunzi wa Kiafrika. Watunzi wenyewe ni Bosco Mulwa, Justus Myello, Dan Mutuku, Kijana Mumo na Wanginga. Wasanii hawa waliteuliwa kimakusudi kutoka jamii ya Wakamba.

Downloads

Published

01-09-2020

Issue

Section

Articles