Ufemerali katika Nyimbo za Muziki wa Bongofleva nchini Tanzania

Mifano kutoka Nyimbo Teule

Authors

  • Steven Yesaya Chuo Kikuu Kishirikishi cha Askofu Mihayo cha Tabora (SAUT-Tabora) Author

Keywords:

Uferemali, Nyimbo, Muziki, Bongofleva

Abstract

Makala haya yamechunguza ufemerali katika nyimbo za muziki wa Bongofleva nchini Tanzania, mifano kutoka katika nyimbo teule za wasanii wa muziki huu ambao nyimbo zao zimeonekana kuwa na ufemerali. Istilahi ufemerali iliyotumika katika Makala haya imetoholewa kutoka lugha ya Kiingereza katika neno “Ephemeral” likimaanisha hali ya kitu kupendwa sana, kuvuma na baada ya muda mfupi kitu hicho kuchuja na kupoteza mvuto au umaarufu wake. Nyimbo za muziki wa Bongofleva zinazotolewa na wasanii zina sifa ya ufemerali yaani pindi zinapotolewa hupedwa sana, huvuma na baada ya muda mfupi huchuja, kupoteza mvuto na umaarufu wake kwa wasikilizaji. Katika jamii ya Watanzania kumekuwa na hali ya vitu, matukio au mtu kuvuma katika muda fulani kisha kuchuja na kupoteza umaarufu wake kutokana na matukio yanayoambatana. Miongoni mwa mambo au matukio yanayoongoza kwa ujitokezaji huu ni pamoja na nyimbo za muziki wa Bongofleva. Data zilizotumika katika Makala haya zilipatikana kwa kutumia njia kuu mbili yaani usaili na ushuhudiaji. Katika Makala haya imebainishwa kuwa sifa ya ufemeralikatika nyimbo za muziki wa Bongofleva, ni kitendo cha kuvuma na kuchuja baada ya muda mfupi. Dhana ya ufemerali inahusisha kitendo cha nyimbo kupendwa, kuvuma na kisha baada ya muda mfupi nyimbo hizo kupoteza mvuto na umaarufu wake. Hivyo Makala haya yameonesha kuwa katika nyimbo za muziki wa Bongofleva imeonekana kuwa dhana ya mawanda mapana ya kupendwa na kuvuma inajitokeza zaidi katika nyimbo za muziki huu ikilinganishwa na aina nyingine ya nyimbo zinazoonekana kuendelea kupendwa licha ya kutungwa na kuimbwa miongo kadhaa iliyopita, mfano nyimbo za muziki wa dansi, maarufu kwa jina la zilipendwa. Ijapokuwa lengo la Makala haya sio kulinganisha nyimbo za muziki wa Bongofleva na nyimbo za muziki wa dansi, dhima ya Makala haya ni kuchunguza ufemerali katika nyimbo za muziki wa Bongofleva kwakumakinikia kuchunguza sababu za ufemerali katika nyimbo za wasanii teule.

Downloads

Published

07-08-2023

Issue

Section

Articles