Usawiri wa Upembezaji wa Mwanamke katika Bunilizi za Clara Momanyi

Authors

  • Kawira Kamwara Chuo Kikuu cha Nairobi Author

Keywords:

Upembezwaji, Ufeministi wa Kiafrika, Ubabedume, Utamaduni, Bunilizi

Abstract

Makala haya yanahusu usawiri wa upembezaji wa mwanamke katika bunilizi za Clara Momanyi. Upembezwaji wa mwanamke ni suala ambalo limekithiri katika jamii nyingi za Kiafrika. Utamaduni hasi na ubabedume ni mambo ambayo yamechangia pakubwa upembezwaji huu. Hata hivyo, kwa kiwango fulani mwanamke mwenyewe amechangia hali hii kwa kujidunisha mwenyewe au kwa kukosa sauti na ujasiri wa kusimama kidete na kujiamulia mustakabali wake. Suala hili limejitokeza katika bunilizi za Clara Momanyi. Katika makala haya, nilihakiki hadithi fupi zifuatazo: ‘Ngome ya Nafsi’ kwenye diwani ya Mayai Waziri wa Maradhi na Hadithi Nyingine (2004) na riwaya ya Tumaini (2006).

Downloads

Published

30-09-2020

Issue

Section

Articles