Uakisikaji wa Udongo kama Suala la Kiikolojia katika Ushairi wa Kiswahili
Mfano katika Ushairi wa Mohammed na Mberia
Keywords:
Uakisikaji, Udongo, IkolojiaAbstract
Makala haya yanachunguza na kubainisha uakisikaji wa udongo kama suala la kiikolojia na linavyochimuza katika tungo za ushairi za Mohamed na Mberia. Ili kutimiza lengo hilo, tumetumia mbinu ya usampulishaji lengwa katika kuteua diwani Kina cha Maisha (Mohamed, 1984), Jicho la Ndani (Mohamed, 2002), Msimu wa Tisa (Mberia, 2007) na Rangi ya Anga (Mberia, 2014). Tungo hizi tumeziteua kwa sababu zinasawiri udongo kama suala la kimsingi la kiikolojia na hivyo basi zinatupa data mwafaka ya kutimiza madhumuni yetu. Hali kadhalika tumechanganua data yetu kwa njia ya maelezo huku tukitoa ufafanuzi na thibitisho kutoka kwa mashairi teule katika diwani za Mohamed na Mberia. Fauka ya haya, tumeongozwa na nadharia ya ikolojia inayotumika kuangazia ukuruba na mwingiliano uliopo kati ya mazingira ya kiasili na binadamu katika tungo bunilizi za kifasihi (Glotfelty, 1996). Baada ya uchunguzi wetu tumebainisha kuwa mashairi ya Mohamed na Mberia yanaakisi suala la uhaianuwai wa udongo kama suala la kiasili na jengwa linalohimili maisha na uhai wa binadamu na viumbe wengine. Mathalan, tumebainisha kuwa kupitia kwa baadhi ya mashairi wanaonyesha udongo kama elementi ya kimsingi katika kuhifadhi spishi mbalimbali za viumbe, kufanikisha mzunguko mdura wa gesi ya kaboni, kufanikisha mzunguko wa virutubishi na mzunguko wa maji. Hata hivyo, kupitia kwa baadhi ya tungo zao, wanaonyesha kuwa kuna visa, mienendo na taratibu za matumizi ya udongo ambazo ni hatarishi na hukwamiza ufanikivu wa mizunguko duara ya ikolojia. Mfano mwafaka wa visa hatarishi vya matumizi ya udongo ni kama vile: mimomonyoko ya udongo, mitelezo ya ardhi na matumizi ya kemikali hatarishi na zisizo salama kukuzia mimea.
References
Baveye, P. na Cowdy, J. (2016). Soil Ecosystem Services and Natural Capital: Critical Appraisal of Research on Uncertain Ground. Front. Environ. Sci. Eng China, 4, 1-49.
Blouin, M. (2013). A Review of Earthworm Impact and Soil Function Ecosystem Services. Eur. J. Soil Sci., 64, 161-182.
Buell, L. (2005). The Future of Environmental Criticism: Environmental Crisis and Literary Study. Oxford: Blackwell Publishers.
Bunpromkul, P. (2019). Ecocriticism: Literary Works, Nature, Ecology and World. Katika S. Chodudompa (Mh.), Contemporary Approaches to the Study of Literature. Bangkok: Stampaya Press.
De Deyn, B. (2017). Plant Life History and Above – Belowground Interactions: Missing Links. Oiks Journal, 126, 497-507.
De Deyn, G; na Kooistral, L. (2021). The Role of Soils in Habitat Creation Maintance and Restoration. Phil. Trans. Soc., 376, 1-9.
Dymond, F. (2014). Long-Term Soil Moisture Patterns in Northern Minnesota Forest. Soil Science Society of America Journal, 78(1), 208-216.
Estok, S. (2007). Theory From the Fringes: Animals, Ecocriticism, Shakespear. Mosaic J., 40(1), 62-72.
Fiere, N., na wenzake. (2013). Reconstructing the Microbial Diversity and Function of Pre-agricultural Tallgrass Prairie Soils in United States. Science Journal, 342, 621-624.
Food and Agriculture Organization. (2015). Status of the Worlds Soil Resources. Inapatikana katika www.fao.org/publications. Ilisomwa tarehe 19 Mei, 2023.
Galloway, N. (2008). Transformation of Nitrogen Cycle: Recent Trends, Questions, and Potential Solutions. Science Journal, 320, 1387-1390.
Gardi, C., na wenzake. (2013). An Estimate of Potential Threats Levels to Soil Biodiversity in EU. Glob Change Bio J.., 19, 1538-1548.
Garrad, G. (2004). Ecocriticism. London: Routledge Publishers.
Glotfelty, C. (1996). Ecocriticism Reader: Landmarks in Literary Ecology. Athens: University of Georgia Press.
Haeise, U. (1997). Science and Ecocriticism. The American Book Review, 18(15), 4-6.
Hongsuwan, P. (2021). Ecocriticism: Toward a New Analytical Approach to Literary Studies and Literary Tourism. Elementary Education J., 20(6), 1470-1476.
Janzen, H. (2006). The Soil Carbon Dilemma: Shall we Hoard it or Use it?’. Soil Biology and Biochemistry, 38(3), 419- 424.
Kibblewhite, M. (2012). Definition of Priority Areas for Soil Protection at a Continental Scale. Eco and Soil, 28, 128-133.
Kuzyakov, Y. na Blagodatskaya, E. (2015). Microbial Hotspots and Hot Moments in Soil: Concept and Review. Soil Biol. Journal, 83, 184-199.
Lal, R. (2004). Carbon Sequestration. Impacts on Global Climate Change and Food Security. Science Journal, 304, 1623-1627.
Li, S., na Wenzake. (2023). Factors Governing Soil Hydrological Function Under Long-Term Tillage Practices: Insight into Soil Water Repelley’. Inapatikana https.//do.org/10.1002/saj.20554. Ilisomwa tarehe 25 Mei, 2023.
Mberia, K. (2007). Msimu wa Tisa. Nairobi: Marimba Publishers Limited.
Mberia, K. (2007). Rangi ya Anga. Nairobi: Marimba Publishers Limited.
Mohamed, S. (1984). Kina cha Maisha. Nairobi: Longhorn Publishers.
Mohamed, S. (2002). Jicho la Ndani. Nairobi: Longhorn Publishers.
Orgiazzi, A., na Wenzake. (2016). Global Soil Biodiversity Atlas. European Commission. Luxembough: Publication Office of the European Union.
Pradittatsanee, D. (2016). Examine Environmental Issues through the Perspective of Contempoarary American Literature. Bangkok: Chulalongkorn University Press.
Robinson, D., na Wenzake. (2013). Natural Capital and Ecosystem Services, Developing Appropriate Soils Framework as a Basis for Valuation. Soil Biology and Biochemistry J., 57, 1023-1033.
Ruekert, W. (1978). Literature and Ecology: An Experiment in Ecocriticism. Lowa Review J., 9, 71-69.
Schlaghamersky, J., na Wenzake. (2014). Earthworm Invasion Alters Enchytraeid Community Composition and Individual Biomas in Northern Hardwood Forests of North America. Appl Soil J., 83, 159-169
Slovic, S. (2000). Ecocriticism: Containing Multitudes, Practicing Doctrine. Katika L. Coupe (Mh.), The Green Studies Reader: From Romanticism to Ecocriticism. London: Routledge Publishers.
Smith, P., na Wenzake. (2013). The Role of Ecosystems and their Management in Regulating Climate, and Soil, Water and Air Quality. Journal of Applied Ecology, 50, 812-829.
Trap, J., na Wenzake. (2016). Ecological Importance of Soil Bacterivores For Ecosystem Function. Eco and Soil Journal, 398, 1-24.
Wall, D. (2012). Soil Ecology Services. Oxford: Oxford University Press.
Whitmore, P., Kirk, J. na Rawlins, B. (2014). Technologies for Increasing Carbon Storage in Soil to Mitigate Climate Change Soil Use and Management. Eco and Soil Journal, 31(51), 62-71.