Misingi ya Mfumo Dume katika Jamii

Mfano wa Wahusika wa Kiume katika Tamthilia ya 'Mke Mwenza'

Authors

  • Mutungi Boaz Chuo Kikuu cha Makerere Author

Keywords:

Mfumo-Dume, Misingi, Uke Wenza, Ufeministi wa Kiafrika

Abstract

Harakati za kumkomboa mwanamke dhidi ya utawala wa kuumeni ni jambo ambalo limedumu tangu miaka ya 1960 ambapo shughuli za Tapo la Ukombozi wa Wanawake zilianza kupamba moto kote duniani. Katika taaluma ya fasihi, nadharia mahususi ya ufeministi iliundwa kwa lengo la kutumia fasihi kama jukwaa la kumuinua na kumkomboa mwanamke. Mojawapo ya malengo ya nadharia hii ni kuwahimiza wanafasihi kuunda mhusika kielelezo wa kike, anayesifika, na mwenye uwezo katika nyanja mbalimbali za kijamii. Je, harakati za Tapo la Ukombozi wa Wanawake pamoja na utekelezaji wa nadharia ya ufeministi yameathirije mfumo dume? Je, wahusika wa kiume bado wababe? Je, mfumo dume umepungua au unakithiri? Makala haya yanalenga kujibu maswali haya kwa kuchunguza sifa na tabia za wahusika wa kiume katika tamthilia ya ‘Mke Mwenza’ ya Nyaigotti-Chacha (1982). Kwa kutumia mkabala wa ufeministi wa Kiafrika, utafiti wetu umegundua kwamba mila, imani na mienendo ya kijadi, na hata ya kisasa inaendelea kumdhalilisha mhusika wa kike, huku akikwezwa mhusika wa kiume. Kwa jumla, mhusika wa kiume bado anadhihirisha mamlaka katika jamii.

Downloads

Published

30-09-2018

Issue

Section

Articles