Mikakati ya Upishaji na Unyakuzi wa Zamu katika Mawasiliano ya Facebook

Authors

  • Bernard Mahero Toboso Chuo Kikuu Kishiriki cha Alupe Author
  • Mosol Kandagor Chuo Kikuu cha Moi Author

Keywords:

Upishanaji Zamu, Mawasiliano, Viashiria, Facebook

Abstract

Upishanaji zamu ni mkakati maarufu katika mawasiliano ya ana kwa ana. Hii ni miafaka ambayo hutawala mawasiliano na kuwasaidia wazungumzaji kuwasiliana bila kuwepo kwa mizozo ya kizamu. Facebook, hata hivyo, ni mtandao unaotawaliwa na mawasiliano ya kimaandishi. Ingawaje ni hivyo, mawasiliano hayo huwa ya kimajibizano kama yale ya mazungumzo ya ana kwa ana. Uatafiti huu unatalii mawasiliano ya Facebook na kuchanganua mbinuĀ  za marafiki za kupishana zamu ya mawasiliano. Matokeo yake yatasaidia kutoa fahamisho la viashiria vya mwisho na mwanzo wa tamko katika mawasiliano ya Facebook ikikumbukwa kwamba mawasiliano ya Facebook ni ya kimaandishi japo yana sifa za mazungumzo ya ana kwa ana.

Downloads

Published

30-04-2018

Issue

Section

Articles