Uchunguzi Linganishi wa Kirai na Neno Ambatani katika Kiswahili
Keywords:
Kirai, Neno Ambatani, Neno KuuAbstract
Kirai ni kipashio cha kisintaksia ilhali neno ambatani ni kipashio cha kimofolojia. Vipashio hivi vya nyanja mbili zinazohusiana vimekuwa vikijadiliwa na baadhi ya wanaisimu kwa mitazamo tofautitofauti. Vipashio hivi hutazamwa kama vipashio tofauti na wakati mwingine hutazamwa kama vipashio vinavyohusiana. McCarthy (2002) anadai kwamba neno ambatani ni kipashio kidogo zaidi ya kirai na kwamba kipashio hicho hubebwa na muundo wa ndani wa kirai. Hata hivyo, anasisitiza kwamba kisintaksia neno ambatani hufanya kazi kama neno na siyo kirai. Kwa upande mwingine, Gichuru (2010) anadai kwamba uhusiano wa maneno yanayounda neno ambatani unashabihiana na uhusiano unaopatikana katika miundo ya kisintaksia kama kirai. Madai haya ndiyo yaliyosababisha raghba ya mwandishi kushughulikia uchunguzi linganishi wa vipashio hivyo. Hivyo basi, makala haya yamelinganisha na kulinganua vipashio hivyo kwa kuzingatia muundo, maana, matamshi, uhusiano wa vijenzi na othografia ya vipashio husika.