Uhalisiamazingaombwe katika Riwaya za Shaaban Robert

'Kusadikika' na 'Kufikirika'

Authors

  • Anna N. Kyamba Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Author

Keywords:

Uhalisiamazingaombwe, 'Kusadikika', 'Kufikirika', Shaaban Robert

Abstract

Uhalisiamazingaobwe ni mkondo wa usasa leo. Ni mkondo uliochipuka huko Amerika ya Kusini miaka ya 1960 licha ya kwamba dalili zake zilikuwako kabla katika hekaya na fasihi simulizi za mataifa mengi zikiwemo za fasihi ya Kiafrika na Kiswahili (Mulokozi, 2017). Abrams (1999) anaeleza kuwa nadharia hii ilianza miaka ya 1920 ambayo mwanzoni ilitumika kuhusu wachoraji na baadaye katika bunilizi za kinathari Bunilizi za kinadhari za Jorge Luis Borges (1899-1986) wa Argentina, na halikadhalika kazi za waandishi kama vile Gabriel García Marquez (1927-2014) wa Kolombia, Isabel Allende wa Chile, Günter Grass (1927-2015) Mjerumani, Italo Calvino wa Italia, na John Fowles (1926-2005) wa Uingereza. Kutokana na mawazo hayo ndipo tunapata kujiuliza maswali kuhusu chimbuko la nadharia hii katika fasihi ya Kiswahili ni lipi hasa? Kusema Kezilahabi ni mwasisi wa mkondo huu ni sawa? Ilihali kulikuwa na kazi za Shaaban Robert zenye vimelea vya nadharia hii. Kutokana na mawazo ya wataalamu mbalimbali tunaona kuna haja ya kuchunguza endapo riwaya za Shaaban Robert zina Uhalisiamazingaobwe au la. Katika uchambuzi huu tutajikita katika kuchunguza riwaya mbili ya Kusadikika na Kufikirika. Riwaya ya Adili na Nduguze itatumika pale tu itakapobidi.

Downloads

Published

30-04-2022

Issue

Section

Articles