Tafakuri ya Upolisemia na Usitiari wa Ungonoshaji wa Maneno katika Kiswahili cha Mazungumzo

Authors

  • Mohamedi A. Ngunguti Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Author
  • Gastor C. Mapunda Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Author

Keywords:

Ungonoshaji, Mazungumzo, Wawasiliani, Polisemia, Sitiari

Abstract

Kumeibuka tabia ya baadhi ya wawasiliani wa Kiswahili kuyapa tafsiri za kingono maneno ambayo hayahusiani moja kwa moja na ngono. Katika miktadha mingi ya kimawasiliano ni jambo la kawaida kwa baadhi ya wawasiliani kukihusisha na ngono chochote kisemwacho; iwe kwa misingi ya viungo vya ngono, mitindo ya ngono, au tendo la ngono. Hali hiyo ndiyo ambayo katika makala hii tunaiita ungonoshaji. Licha ya kuwapo kwa viashiria vya kusambaa kwa ungonoshaji, nafasi yake kiisimu bado haijafahamika. Hilo ndilo lililoibua haja ya kufanya utafiti huu kwenye Kiswahili cha mazungumzo, huku tukijiuliza iwapo ungonoshaji unahusiana na polisemia au sitiari. Chanzo cha data za makala hii ni maktabani ambapo data zilikusanywa kwa mbinu ya uchanganuzi wa nyaraka. Data hizo zilihusisha kauli mbalimbali zenye viashiria vya ungonoshaji zilizosemwa na watu mbalimbali na kunukuliwa na kuhifadhiwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii katika mfumo wa sauti au video. Mitandao ya kijamii tuliyoiteua na kuitumia ilikuwa Youtube, Instagram na Facebook. Makala hii basi imebaini kuwa, kwa kiasi kikubwa, ungonoshaji wa maneno katika Kiswahili cha mazungumzo kwa kiasi kikubwa una sitiari ingawa polisemia pia hujitokeza.

Downloads

Published

30-09-2021

Issue

Section

Articles