Taasubi katika Shirikana za Kivumba

Mtazamo wa Kisemiotiki

Authors

  • Sanja L. W. Leo Chuo Kikuu cha Nairobi Author

Keywords:

Shirikina, Kivumba, Semiotiki, Taasubi, Ishara

Abstract

Makala haya yanachunguza baadhi ya shirikina za Kivumba kwa nia ya kubainisha ya kwamba, zinaashiria kuwepo kwa taasubi ya kiume katika jamii husika. Hakuna usawa wa kijinsia katika masuala kama vile malezi ya watoto na ulaji wa vyakula hasa kwa mwanamke. Ili kukuza mjadala wetu, makala yamefafanua ishara na maana kama zinavyojidhihirisha katika baadhi ya mifano ya shirikina za Kivumba. Makala haya yanachukulia kwamba sio rahisi kufasiri ishara na maana katika shirikina za jamii yoyote nje ya mkutadha wa jamii hiyo. Ushahidi wote unaotegemewa katika mjadala wetu ulitokana na mifano iliyokusanywa kutoka nyanjani.

Downloads

Published

30-09-2020

Issue

Section

Articles