Dhanagande na Vichekesho vya Kikabila kama Lugha ya Chuki
Keywords:
Dhanagange, Ukabila, Vichekesho, ChukiAbstract
Nchi ya Kenya ina zaidi ya makabila 42. Wakenya wengi hujitambulisha na jamii zao. Kwa muda sasa, kila jamii imeundiwa dhanagande pamoja na vichekesho vinavyohusiana nayo. Makala haya yanashughulikia uhusiano uliopo baina ya dhanagande, vichekesho vya kikabila, na chuki za kikabila; mada ambayo haijashughulikiwa na watafiti wengi. Aidha, makala haya yanaupima utani huu katika mizani ya sheria za nchi ya Kenya ili kuona kama kuna ukiukaji wowote unaotokana na athari zake. Makala yanaonesha kwamba vichekesho vya kikabila vinavyokiuka mipaka si mzaha tena bali ni namna nyingine ya kueneza chuki. Nadharia zinazotumiwa kuchanganua mada hii ni zile za Majikwezo, Kutopatana kwa mawazo na ile ya Faraja (Raskin, 1985). Nadharia hizi huweza huzingatia madhumuni mbalimbali ya vichekesho. Data ya makala imetolewa kwenye mitandao ya kijamii na pia kutoka kwa kipindi cha Churchill Show. Makala yanaweka wazi changamoto za kisheria katika kukabiliana na hali hii. Pia kunatolewa mapendekezo ya namna ya kukabiliana na hali kama hizi kwa ajili ya utangamano wa kitaifa.